Navigate / search

Dalili Za Watu Wanaoishi Ili Kuwafurahisha Wengine-Je,Unazo?

Multi-ethnic men talking to bored woman

Dr.Daniel Amen,aliwahi kutengeneza kanuni maarufu sana iliyojulikana kama 18/40/60.Katika kanuni hii alieleza kuwa mtu anapokuwa na miaka 18 huwa kila wakati anawaza watu wanafikiri nini juu yake,hivyo kwa kila anachofanya akili yake huwa inajiuliza kuwa “Hivi watu watasemajae?”.Lakini mtu huyohuyo akishafikisha miaka 40 huwa hajali watu wanasemaje,hivyo huamua kufanya mambo bila kuyumbishwa na wazo la kufikiria kuwa watu wanawaza nini juu yake.Cha ajabu ni kuwa mtu huyo akifikisha miaka 60 anakuja kugundua kuwa katika muda wote huo wa maisha yake hakuna mtu aliyekuwa anamfikiria yeye,kiufupi ni kuwa kila mtu alikuwa anajifikiria mwenyewe.

Hakuna hasara kubwa unayoweza kuipata katika maisha yako kama kupoteza muda wako wote katika maisha yako kisha ukaja kugundua kuwa uliokuwa unajaribu kuwafurahisha na kuwaridhisha hawakuwa hata na muda na wewe.Ili kufanikiwa katika maisha yako ni lazima uamue kuishi maisha ambayo haupotezi muda kuwaza watu huwa wanakufikiriaje ama watasemaje kuhusu wewe.Hata hivyo ni rahisi sana kujua kama unaishi kwa kuwaridhisha wengine ama unaishi kwa kuifuata ndoto yako kwa kuangalia dalili zifuatazo:

Moja,kama wewe ni mtu ambaye unapenda kumiliki vitu vyenye gharama kubwa kuliko uwezo wako wa sasa.Kila mtu anatamani kuwa na vitu vizuri,hiyo inaeleweka,ila lazima viendane na uwezo wa kipato chako.Namna pekee ya kujua kuwa unajaribu kuishi zaidi ya uwezo wako ni kuwa kila wakati utakuwa unakopa ili kununua vitu visivyo vya lazima(luxuries) kama vile nguo,viatu n.k.Ingawa watu watakuwa wanakusifia lakini wewe utakuwa unajua ndani yako jinsi unavyoumia ili kuweza kuendelea katika aina hiyo ya maisha.

Pili ni kuwa utakuwa ni mtu wa kujionyesha sana(show off).Kwa kawaida watu wanaoishi kwa kuwapendeza wengine huwa hawana “self-approval”-Hawajikubali hadi wakubaliwe na watu wengine.Kwa sababu hiyo huwa ni watu wa kujitahidi sana kutafuta kusifiwa au kuambiwa neno la kukubaliwa.Katika ulimwengu wa mitandao hawa ni rahisi sana kuwajua,watataka kuonyesha kila kitu wanachofanya,walichovaa,wanachokula n.k.Kiufupi ni kuwa wanaamini kuwa kadiri watu wengi wanavyowasifia au kulike mambo yao basi ndio wanapata furaha Zaidi.

Dalili ya tatu,huwa ni watu wanaopenda kujionyesha wanajua kila kitu.Watu wa namna hii hupenda kuonekana ni wa muhimu kuliko inavyotakiwa ama kuliko hadhi yao.Kila mada kuanzia physics hadi medicine utawakuta wanabishana na wanataka kuonekana wanajua kuliko mtu yoyote.Huwa wanajua kuanzia siasa hadi mambo ya madini,wanataka kuchangia kwenye kila kitu na wanataka kumuonyesha kila mtu wanajua kila kitu;huwa si wepesi wa kusikiliza bali ni wepesi wa kusema Zaidi.Huwa wanaamini ili wakubalike na wapendwe na wengi basi inatakiwa waonyeshe wanajua kila kitu.
Mwisho ni kuwa huwa watu ambao wako tayari kuwasema wengine vibaya ili mradi kwa kufanya hivyo itawafanya wapendwe na wale wanaozungumza nao kwa wakati huo.

Kukiwa na mazungumzo yanayomhusu mtu fulani na ghafla ikapatikana na nafasi ya kuzungumza mabaya ya mtu huyo,watu wa namna hii huharakisha kusema vibaya wengine ili wao waonekane wazuri.Wako tayari kubomoa sifa ya mtu aliyoijenga kwa miaka ili wao wapate sifa ya muda.Watu wa namna hii wako tayari kuchafua wengine hata kama wanayosema hawana uhakika nayo ama hayakuwa lazima kuyasema.

Ili ufanikiwe katika ndoto yako ni lazima uamue kuwa ndoto yako ndio kitu cha muhimu zaidi kuliko kitu chochote kile,usiwe mtu ambaye anaishi ili kupendezesha wengine na mwisho wa siku ukajilaumu kuwa umepoteza muda kuwaridhisha watu ambao hawakuwahi kujali kuhusu ndoto Yako.Be Focused!

Kumbuka maneno ya Bill Cosby aliyesema-Sijui sir ya mafanikio bali najua siri ya Kufeli,ni kkujaribu kumfurahisha kila mtu.(I don’t know the secret to success,but the secret to failure is tyring to please everybody)

Kumbuka kuwa ndoto yako ianwezekana.

Endelea kutembelea ukurasa wangu wa facebook ili kujifunza zaidi.

See You At The Top.A

Comments

joram mwangosi
Reply

waooooooooh…it has been helpful to me
blessed

Leave a comment

name*

email* (not published)

website