Navigate / search

Mambo 3 Yaliyomsaidia Manny Khoshbin Kutoka Kulala Nje Hadi Kuwa Na Biashara Zake

 

Manny Khoshbin ni mmoja kati ya watu wengi sana ambao wameanzia chini kabisa katika masiha yao na leo wamefika hatua nzuri.Aliingia marekani akiwa na umri wa miaka 14 baada ya kukimbia kutoka katika nchi yake ya Irani ambako kulikuwa na machafuko makubwa sana.

Alipofika marekani alikuwa hawana pesa kabisa na alikuwa hana mahali pa kulala hiyvo iliwalazimu wawe wanalala kwenye gari kabla ya kupata msaada Read more

ADUI WA 4: Kukosa Maarifa Yanayotakiwa

Siku zote kiwango cha mafanikio yako kinatokana na kiwango cha maarifa uliyonayo juu ya jambo unalolifanya.Kuwa na malengo na bidii peke yake haitoshi juu ya kile unachofanya,ni lazima ujikite kuwa na maarifa ya kiwango cha juu sana katika kile unachofanya.Itashanagza sana kama wewe unataka kuwa mfanyabishara mkubwa sana lakini kila siku kazi yako ni kusoma magazeti ya udaku tu ama ni kuangalia novie tu.Kama unataka kuwa mfanyabishara mkubwa ni lazima ujikite katika kutafuta elimu na maarifa yahusuyo biashara,tafuta historia za wafanyabiashara waliofanikiwa usome historia zao,ujue vikwazo walivyokutana navyo,ujue mbinu walizotumia kufanikiwa na kukuza makampuni yao. Read more

Mambo Mawili Ya kufanya Ndoto Yako Inapoonekana Haiwezekani Kufanikiwa

Kwenye maisha yangu nimeshawahi kupitia wakati ambapo niliona kama vile ndoto yangu na malengo ambayo ninayo kwenye maisha ni kama vile hayataweza kufanikiwa tena.Hali hii sio tu mimi ambaye imewahi kunitokea,niliposoma habari za watu wengine nilikuja kugundua kuwa na wao pia wamepitia sana hali kama hizi na wengine ni mbaya zaidi kuliko ambazo sisi tumewahi kuzipitia,ila kilichowasaidia ni uamuzi wao wa kukataa kukata tamaa.

Read more

Mambo 3 Ya Kuyazingatia Ili Ufanikiwe Kazini Kwako

Ili kufanikiwa katika kazi unayoifanya unahitaji zaidi ya ujuzi wa kawaida wa kufanya kazi.Wako watu wengi sana ambao wameshindwa kuzingatia mambo muhimu yanayoonekana kuwa ni madogo lakini ambayo yanaweza kukufanya ufanikiwe ama ufeli kwenye kazi ambayo unaifanya.Leo nataka uyatambue mambo 3 muhimu ambayo kila mahala unapokuwa unaanza kufanya kazi ni lazima uyazingatie kama unatakiwa kufanikiwa katika kazi hiyo.
Jambo la kwanza kabisa ni kujifunza utamadami wa kampuni au shirika jipya ambalo unaanza kulifanyia kazi.Kila taasisi huwa ina utamadami wake ambao kwa kawaida huwa unatofautiana na wengine.Hii inamaanisha kama haujui utamaduni wa mahali Read more

Sababu Kuu 3 Zinazosababisha Watu Kughairisha Mambo

Takribani 80% huwa wanaacha kuendelea na mipango yao waliyojiwekea baada tu ya miezi mitatu ya kwanza mwaka unapoanza.Hii imewafanya watu wengi sana kujikuta wakiwa na hamasa na shauku kubwa mwaka unapoanza na kujikuta shauku yao ikiishia njiani.Unaweza kujikuta kuwa wewe ni mtu ambaye kila mwaka huwa unaanza mwaka kwa kishindo lakini baada ya muda kidogo tu unajikuta umeshakata tamaa na hauendelei tena na kufuatilia utekelezaji wa malengo yako.
Ili usiwe mmoja wa wale ambao kila wakati huwa wanaghairisha mambo na hujikuta wanaanza upya kila wakati ni lazima ujue sababu zinazowafanya watu wengi kuwa na tabia hiyo na wewe ujigundue huwa unaghairisha mambo kwa sababu zipi na ujue namna ya kujitoa kutoka katika tabia hiyo:
Sababu ya kwanza ni kusubiri kuwa na kitu kikubwa ili waanze kufanya kile ambacho wanataka kukifanya.Tatizo kubwa sana ambalo watu wengi sana limewakwamisha ni tabia ya kusubiri kuwa na vingi.SIku zote kumbuka kuwa hauwezi kuwa na vingi kama vile vichache ambavyo unavyo umeshindwa kuvitumia kwa ufanisi.Siku zote kama wewe utakuwa ni mtu wa kudharau kile kidogo ulichonacho basi hautaweza kupata kikubwa unachokitafuta.Kila wakati jiulize-Hivi katika hiki kidogo nilichonacho nitaweza kuanza Read more

Jinsi Ya Kujenga Ujasiri Kwenye Kila Unalofanya

Uwezo wako wa kujiamini na kuwa jasiri kufanya kile ambacho unataka ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa katika malengo uliyonayo.Kuna watu wengi sana ambao wamepoteza fursa kubwa sana katika maisha kwa sababu walikosa ujasiri,
kuna watu ambao walishindwa kujielezea ili wapate wanachotaka kwa kukosa ujasiri,kuna watu ambao wameshindwa kuanza kufanya kitu wanachokitamani kwa kukosa ujasiri,kuna watu ambao wamefeli usahili wa kazi kwa kukosa ujasiri,kuna watu wameogopa kufanya maamuzi muhimu kwenye maisha yao na matokeo yake wamedumaa mahali pamoja na wanaishi kwa “stress” za hali ya juu kwa sababu ya kukosa ujasiri wa kufanya maamuzi.

Sifa mojawapo ya watu ambao wanafika mbali sana ni wajasiri katika yale ambayo wamekusudia kuyafanya.Huwa wanapoamua kufanya kitu wanachukua hatua bila kuogopa.Kuna watu wengi sana kwa kukosa ujasiri wamejikuta wamekubali kujiingiza
katika “Commitments” ambazo  hawakuwa tayari kuzitekeleza ila kwa sababu ya hofu na uoga wakajiingiza.Kuna watu ambao wamesema ndiyo katika mambo ambayo walikuwa wanatamani kusema hapana na baadaye wakajikuta katika matatizo makubwa sana.Leo nataka ufahamu mambo kadhaa kuhusu hofu katika maisha yako:

Kwanza ni kujua kuwa kila mtu unayemuona ni jasiri katika jambo fulani kwenye maisha yake,kuna siku aliwahi kupata hofu ya jambo hilo.Kila unayemuona leo anasimama mbele za watu na anaongea kwa ujasiri kuna siku alikuwa muoga na alipoitwa mbele za watu pengine alitokwa na jasho jingi kwa uoga.Kila unayemuona huwa akitaka kitu Read more