Navigate / search

Umekuja Duniani Kufanya Nini?:Mambo 4 Ya Kuyafahamu kuhusu Kusudi Lako La Kuzaliwa

 

beach-838803_960_720

Utafiti ambao uliwahi kufanywa na taasisi ya moyo ya marekani(American Heart Association) uligundua kuwa watu wengi hupata magonjwa ya moyo na kufariki siku ya jumatatu asubuhi.Hii ni kwa sababu baada ya mapumziko ya weekend wanajikuta wanatakiwa kulazimika kwenda kufanya kazi ambazo wanazichukia na ambazo kama wangekuwa na namna nyingine wangeacha kabisa kuzifanya.Pengine hata leo unaposoma Makala hii,upo katika hali ya kufanya kitu ambacho hukipendi na unajilazimisha tu kufanya na pengine ungetamani kufanya kile unachokipenda ila hauwezi. Read more

Sauti Ya Patrice Lumumba Bado Inasikika-Nani ataitikia Wito?

Patrice-Lumumba3

Leo nilimkumbuka shujaa wa nchi ya Kongo DRC,Patrice Lumumba nikaamua kuirudia kuisoma barua yake ambaye alimwandikia mke wake Pauline na watoto wake muda mchache kabla hajauwawa mwaka 1960.Ni barua ambayo siku ya kwanza nilipoisoma miaka kadhaa huko nyuma ilinitoa machozi sana.

Katika barua ile alimwambia mke na watoto wake kuwa hana uhakika kama barua ile itawafikia lakini pia hana uhakika kama ataweza kuwaona tena.Juu ya yote alieleza kuwa anajisikia fahari sana kwa kuwa hayuko tayari kuwa kibaraka wa kikoloni na kuwasaliti wananchi wa kongo kwa jambo lolote lile,yuko tayari kufa ili mradi anasimamia jambo sahihi kwa manufaa ya wengi.

Barua hii inanikumbusha maneno ya Emiliono Zambata,kamanda wa jeshi na mwanamapinduzi wa mexico aliyesema”Ni bora kufa umesimama kuliko kuishi huku umepiga magoti”.Ghafla nikakumbuka maneno ya mwanaharakati Read more

Je,Kuna Siku Itafika Nawe Utatoa Machozi Kama Alix?

alix-idrache-2

Umeshawahi kufanikiwa katika jambo ambalo ulikuwa unaona kama vile haliwezekani?Ama umeshawahi kuvuka kikwazo ambacho kilikuwa kinaonekana kinatishia mafanikio yako ya kesho?Umeshawahi kuwa katika hali inayoonyesha kuwa hautaweza kuinuka tena lakini ghafla unashangaa umefanikiwa kuvuka kikwazo kilichokuwa kinakukabili?

Gazeti la Bussiness insider la tarehe 26,May 2016 liliripoti habari iliyokuwa inasisimua na yenye mafunzo makubwa sana kuhusu mafanikio katika maisha ya kila siku. Second Lt. Alix Schoelcher Idrache hakuwahi kufikiria kuwa kuna siku ambayo ndoto yake ya kumaliza mafunzo ya kijeshi na kufanikiwa kwa kiwango cha juu itatimia.Picha zilisambaa zikimwonyesha Read more

Jifunze Toka Kwa Rosa Parks:Namna Ya Kutengeza Historia Mpya Maishani Mwako

rosa-parks-wisdom

Mchana wa tarehe moja desemba mwaka 1955 mama mmoja wa miaka 42 mmarekani mweusi aliyejulikana kwa jina la Rosa Parks, akiwa anarudi nyumbani kutoka kazini kwake Montgomery, Alabama, ambako alikuwa anafanya kazi kama fundi msaidizi wa ushonaji alipanda basi namba 2857 eneo la Cleveland.Akiwa tayari amekwisha kaa,akaja akaambiwa ainuke ili ampishe mzungu akae,akakataa na ndipo alipokamatwa kwa kuvunja sheria ya ubaguzi wa rangi ambayo ilkuwa inatumika wakati huo.Kitendo chake hicho ndicho kilipelekea mgomo wa waafrika kugomea mabasi kwa miezi 13 na kupitia mgomo huo ulioongozwa na Martin King Jr ndipo hekaheka za kutafuta haki za weusi marekani zilipamba moto. Read more

Jifunze Kwa Annie:Binti Milionea Aliyeacha Kuajiriwa na Kuanza Kilimo

wpid-annienyaga1

Annie Nyaga amefanya kitu ambacho kimebadiisha fikra za watu wengi hasa vijana wa kiafrika,na hii ilikuja baada ya jina lake kuchomoza katika orodha ya vijana mamilionea nchini Kenya wakati huo akiwa hajulikani na mtu yeyote kabisa.Akiwa na digrii yake ya kwanza ya Biomedical Science and Technology kutoka chuo kikuu cha Egerton aljikuta amekataa scholarship aliyopewa ya kwenda kusoma Marekani ili aiishi ndoto yake ya kuwa mkulima.Annie wakati ameibuka kuwa milionea alikuwa ni binti kijana wa miaka 29 lakini maisha yake yamebadilika sana kwa kuamua kuishi kitu ambacho moyo wake ulikuwa unakitamani kila siku. Read more

Tabia 10 Za Vijana Waliofanikiwa Kuwa Mabilionea Duniani

0x600

Wengi wetu, katika nyakati tofauti, tumewahi kujenga picha juu namna gani maisha yanaweza kuwa kama tukiwa na utajiri mwingi sana-malumu kabisa, pengine katika kiwango dola bilioni. Watu watafanya kazi maisha yao yote lakini hawafikii lengo hili , kuna baadhi ambao wanafanikiwa kulifikia lengo hili kabla hawajafika miaka thelathini. Kwa hiyo, hawa watu wanaofanikiwa sana wana kitu gani? Suzy Smith aliwahi kufanya utafiti wake na akagundua tabia kumi ambazo mabilionea wote vijana wanazo. Read more

Mambo 6 ya Kuyazingatia Kabla ya Kuanza Biashara yako Mwenyewe.

buildings-003-big

Nina uhakika nyote mnatambua kuwa kuna umbali mkubwa kati ya wazo zuri na mwanzo mzuri. Lakini watu wengi hawajui namna kujenga daraja kuziba pengo hilo. Watu wamefeli kwenye biashara zao waliozoanzisha kwa sababu hawakutakari vya kutosha juu ya vitu vya muhimu vya kuzingatia kabla ya kuanza.

Leo, nataka nikushirikisha vitu vya mhimu ambavyo unapaswa kuvizingatia kabla ya kuingia kwenye biashara kama namna ya kujiari: Read more

Mambo 2 Ya Kufanya Unapopitia Kipindi Kigumu Maishani

index

Gazeti la the daily mail la uingereza siku ya tarehe 10 Mei lilirpoti taarifa iliyovutia hisia za wengi ulimwenguni.katika toleo hilo lilieleza juu ya kisa cha mwananmke mmoja ambaye ana umri wa miaka 72 na mume wake ana umri wa miaka 79 wamefanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza kwa njia ya IVF baada ya kudumu katika ndoa kwa muda wa miaka 46.

Dr.Arnuragi Bishnoi aliyekuwa anamuhudumia mwanamke huyo kwa muda wa miaka miwil mfululizo katika clinic yake,alikiri kuwa ndoto ya mama huyo kupata mtoto ilikuwa kama ni kizungumkuti cha karne na aliendelea Read more

Umeumbwa Kuwa Tai Usijiruhusu Kuishi Kama Kuku

index

Siku moja nilisoma habari iliyosisisimua moyo wangu na kunifanya nifanye maamuzi mapya kuhusiana na aina ya maisha ninayotaka kuyaishi kuanzia siku hiyo.Kulikuwa na mfugaji mmoja ambaye alikuwa anafuga kuku wengi kijijini,siku moja kwa bahati mbaya aliokota yai la tai akiwa njiani kutoka shambani.Akaamua kulichukua yai lile na akaliweka kwa kuku mmoja wapo ambaye alikuwa anaatamia mayai yake.

Baada ya muda kupita,kuku yule aliyatotoa mayai yale likiwemo na lile yai la tai.Hivyo tai akazaliwa pamoja na vifaranga wengine bila kujua kuwa yeye ni tai.Miaka mingi ikapita bila yule mtoto tai kutambua kuwa ana uwezo wa kuruka juu sana na ana nguvu ya kula vyakula “fresh” na sio kukimbilia katika mashimo ya taka kama wanavyofanya kuku wengine.

Siku moja akiwa anaendelea kutafuta chakula kwa kuparua chini TAI mkubwa akapita akiwa anaruka kwa madaa.Mtoto wa tai akawaambia vifaranga wenzake Read more