Navigate / search

Buster Douglas:Kama Nilimshinda Tyson,Nawe Tumia Mbinu Hizi Utimize Ndoto Zako.

Mike Tyson is knocked out by challenger James "Buster" Douglas (2nd R) during their heavyweight title bout in Tokyo in this photo taken by Kyodo February 11, 1990. Mandatory Credit REUTERS/Kyodo (JAPAN) ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE HAS BEEN SUPPLIED BY A THIRD PARTY. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. MANDATORY CREDIT. JAPAN OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN JAPAN. THIS PICTURE IS DISTRIBUTED EXACTLY AS RECEIVED BY REUTERS, AS A SERVICE TO CLIENTS - RTR4O5AX
Mike Tyson is knocked out by challenger James “Buster” Douglas (2nd R) during their heavyweight title bout in Tokyo in this photo taken by Kyodo February 11, 1990.

Tarehe 11 February 1990 Katika jiji la Tokyo,Japan kulitokea tukio ambalo lilijenga historia duniani.Hii ilitokana na pambano kubwa la masumbwi lililofanyika kati ya Mike Tyson na Buster Douglas.Wakati pambano hili linafanyika Tyson alikuwa ni bondia wa kuogopwa na wa kutisha ambaye alikuwa akishinda kwa KO katika kila pambano lake lililopita,hivyo kila mtu hakuwa na shaka kuwa Tyson angeibuka mshindi kabla raundi tatu hazijamalizika kama iilvyokuwa kawaida yake.

Mara baada ya kuanza pambano kama kawaida Tyson alitumia uwezo wake na nguvu zake kumshambulia adui yake kwa nguvu na kwa masumbwi makali akitarajia kumuangusha na kumshinda katika raundi za mwanzo.Cha kushangaza hadi raundi ya nane inafika mpinzani wake alikuwa bado amevumilia na bado anaendelea kupigana.Ilipofika raundi ya nane Tyson alimpiga ngumi ya katafunua (Uppercut) mpinzani wake na alianguka kwa anguko ambalo hakuna mtu alitarajia atainuka tena.Lakini wakati Tyson anaanza kufurahia kuwa ameshinda,akashangaa Buster Douglas anainuka na akaja na nguvu mpya na ilipofika raundi ya 10 akamshinda Tyson kwa KO na kuweka historia kuliko matarajio ya watu wengi.

Miaka 25 baadaye,Douglas alihojiwa na kuulizwa ni nini kilimfanya ashinde pambano lile,majibu yake yanatoa funzo kubwa sana.

Anasema wakati amesaini kupigana na Tyson mama yake alikuwa anaumwa sana na kabla tu ya pambano alifariki na kabla hajafariki alimwambia kuwa zawadi kubwa anayoweza kumpa ni kumshinda Tyson.Lakini pia,kipindi anaenda kupigana na Tyson alikuwa ametoka kuachana na mke wake na maisha yake tya kifedha yalikuwa na hali ngumu sana,hivyo kumshinda Tyson ilikuwa ni fursa muhimu kwake kubadilisha maisha yake.Hivyo ushindi wake ulianzia kwenye “SABABU” hizi.Douglas anasema ili ufanikiwe hata pale watu wanapofikiri hauwezi kufanikiwa,kitu cha kwanza ni kuwa na sababu(why) yenye nguvu kuliko kuanza kuwaza utafanikiwa kwa namna gani(How).Ili mradi sababu yako(Why) ina nguvu basi namna(How) lazima itapatikana.
Lakini pia,wakati ameanguka chini na akaona kuwa kama ameishiwa nguvu kabisa za kuinuka tena,maswali mengi yalipita ndani yake.Je,niendelee?Lakini mbona nimeishiwa nguvu?Hata hivvyo nimejitahidi nimepigana hadi raundi hii nikiacha hapa nimefanikiwa pia n.k Lakini mara baada ya kukumbuka sababu yake(why) akaamua kuamka kuendelea bila kujali atashindaje(how).Douglas anasema mara baada ya kuamka aliona macho ya Tyson yakikata tamaa kwani hakuamini kama anaweza kuinuka tena;na kwa maelezo yake anasema hapo ndipo alipomshinda Tyson.

Kwenye maisha huwa tunapita katika majira kama haya ambapo inaonekana kama yanayotukabili ni mazito kuliko tunavyoweza kuyashinda,matokeo yake tunakata tamaa kwani kila mtu anatuambia hatutaweza.Lakini tusichojua ni kuwa kama tutapata sababu nzito inayotusukuma kuiishi ndoto yetu,hatutajali changamoto zinazotukabili.Je,una sababu nzito(why) inayokusukuma kuiishi ndoto yako?Kumbuka uzito wa SABABU yako ndio itajulisha kama utafanikiwa ama la.

Lakini pia,tunapokuwa tumeanguka chini kiuchumi,kibiashara,kimahusiano,kielimu na tunaona kama vile hatuwezi kuinuka tena.Huwa maswali mengi yanapita katika katika akili yetu-Hivi itawezekana tena?,Si bora niache tu,nimejaribu kila namna imeshindikana,sitaweza kuinuka tena,kwa kweli nimeishiwa nguvu na kila mtu anajua hilo n.k.Tusichojua ni kuwa kama ilivyokuwa kwa Douglas,mara tutakapoamua kuinuka wakati bado maumivu ni makali na hali inoenekana imeshindika, ndivyo Tyson wetu atakavyokata tamaa ya kuendelea kutushinda.

KUMBUKA:Ushindi wako uko kwenye uwezo wako wa kuinuka na kuendelea pale ambapo kila mtu aliona kwamba hautaweza kuinuka na kufanikiwa tena.
Leo,Usikubali kuogopa kumkabili Tyson wako,Usikubali Kubakia chini baada ya kuangushwa na changamoto zako.Hata kama bado maumivu uanyasikia,bado nguvu hazijarudi,Inuka na uanze upya kuifukuzia ndoto Yako na utashinda.Inawezekana.

Endelea kutembelea www.JoelNanauka.Com ili kujifunza Zaidi.

Ndoto Yako Inawezekana.

See You At The Top

Leave a comment

name*

email* (not published)

website