Navigate / search

Jinsi Ya Kujenga Msingi Wa Mafanikio

Siku moja mwandishi mmoja wa habari alikuwa akimhoji Muhamadi Ali,bingwa wa ngumi za uzito wa juu wa wakati huo na akamuuliza kutaka kujua nini huwa kinamtia hamasa zaidi katika kufanya mazoezi kwa bidii.Jibu lake lilikuwa linafurahisha sana pale aliposema-“Kila siku huwa nikitaka kwenda kufanya mazoezi huwa nasikia uchovu na natamani kuendelea kulala,ila huwa najiambia,ni bora niishi kwa sasa kama mtumwa ili nije kuishi kama mfalme hapo baadaye”.Fikra ya namna hii ndio ilimsaidia kufika kule ambako alikuwa anataka kwenda.

Read more

Hatua 3 Za Kukutoa Kwenye Changamoto Unayoipitia Kwa Sasa

Umeshawahi kupitia hali ambayo kila dalili inaonyesha kwamba hautaweza kuinuka tena?Namaanisha mazingira ambayo hata kwa kila anayekuangalia anajua kabisa kuwa hata kama anakutia moyo,hakuna namna unaweza kufanikiwa.Hali hii huwa inaweza kutokea baada ya mtu kuwekeza katika kitu fulani alichokiamini kwa nguvu zote na kisha anakuja kupata hasara ambayo hakuitegemea kabisa,inaweza kutokea pale ambapo mtu uliyempenda sana na kumwamini siku zote anafanya kitu ambacho haukutarajia na kinakuumiza sana moyo,huwa inatokea pale mtu anapopoteza mtu wake wa karibu sana kwa kifo,huwa inatokea pale ambapo unakuwa umefanya kwa bidii kila unachoweza lakini hauoni matokeo,huwa inatokea pale ambapo unaona watu wanaokuzunguka wanafanya kama yaleyale ambayo wewe unayafanya ila hamna matokeo kabisa,huwa inatokea pale ambapo umebakia peke yako na machozi yako hakuna wa kuyafuta,inaweza kutokea pale ambapo umepewa taarifa kuwa ugonjwa wako hauna tiba. Read more

Hatua 3 Za Kufeli Na Jinsi Ya Kuziepuka

Kila mtu huwa anaogopa kufeli katika kile anachokifanya.Kwa sababu hii kuna watu wengi sana ambao wameshindwa kupiga hatua katika maisa yao kwa sababu ya hofu ya kufanya kitu kipya ambacho kingeweza kuwasaidia kupiga hatua moja mbele kwenye maisha yao.

Hata hivyo kuna watu pia ambao kila wakati wanajikuta wanafeli na kushindwa kuendelea mbele kwenye maisha yao wka sababu huwa hawako tayari kutafakari na kutathmini mambo ya msingi ambayo yaliwafanya washidnwe kuendelea mbele katika kila ambacho wanataka kukifanya. Read more

Njia Moja Ya Kuongeza Thamani Katika Siku Yako

Siku moja muhudumu wa mgahawa wa AppleBees ulioko Texax Kasseys Simons,alikuwa amepitia kwenye Supermarlek kufanya manunuzi kaba hajaingia katika zamu yake kazini.Wakati akiwa kwenye mstari akashangaa kumuona mwanamama mbele ya mstari akiwa analia.Akiwa ananona ndio njia nzuri ya kuweza kumfariji,aliamua kumlipia kaisi cha dola 17 za bidhaa ambazo alikuwa amenunua lakini pia alimpa mawasiliano yake na kisha alimkaribisha katika mgahawa aliokuwa anafanyia kazi kama angependa kupata kahawa pamoja naye. Read more

Mambo 3 Ya Kuyafanya Kila Siku Asubuhi Ili Uwe Na Siku Ya Mafanikio

Jinsi ambavyo huwa unaianza asubuhi yako huwa inapelekea namna ambavyo utafanikiwa katika siku hiyo ama la.Kama wewe ni mtu ambaye unaianza siku yako vibaya basi uanweza kujikuta unaharibu kila hatua ambayo inafuata ndani ya siku hiyo.

Moja ya kitu cha muhimu sana ni kujua kwa ufasaha ni mambo gani unatakiwa kuanza nayo ili siku yako iwe na mafanikio makubwa.Kuna mambo matatu ambayo leo ningetaka uyazingatie unapoanza siku yako ili uifanye siku yako iwe ya mafanikio:

Read more

Mambo Mawili Ya kufanya Ndoto Yako Inapoonekana Haiwezekani Kufanikiwa

Kwenye maisha yangu nimeshawahi kupitia wakati ambapo niliona kama vile ndoto yangu na malengo ambayo ninayo kwenye maisha ni kama vile hayataweza kufanikiwa tena.Hali hii sio tu mimi ambaye imewahi kunitokea,niliposoma habari za watu wengine nilikuja kugundua kuwa na wao pia wamepitia sana hali kama hizi na wengine ni mbaya zaidi kuliko ambazo sisi tumewahi kuzipitia,ila kilichowasaidia ni uamuzi wao wa kukataa kukata tamaa.

Read more

Mambo 3 Ya Kuyazingatia Ili Ufanikiwe Kazini Kwako

Ili kufanikiwa katika kazi unayoifanya unahitaji zaidi ya ujuzi wa kawaida wa kufanya kazi.Wako watu wengi sana ambao wameshindwa kuzingatia mambo muhimu yanayoonekana kuwa ni madogo lakini ambayo yanaweza kukufanya ufanikiwe ama ufeli kwenye kazi ambayo unaifanya.Leo nataka uyatambue mambo 3 muhimu ambayo kila mahala unapokuwa unaanza kufanya kazi ni lazima uyazingatie kama unatakiwa kufanikiwa katika kazi hiyo.
Jambo la kwanza kabisa ni kujifunza utamadami wa kampuni au shirika jipya ambalo unaanza kulifanyia kazi.Kila taasisi huwa ina utamadami wake ambao kwa kawaida huwa unatofautiana na wengine.Hii inamaanisha kama haujui utamaduni wa mahali Read more

Ufanye Nini Unapokatishwa Tamaa-Jifunze Toka Kwa Derek

Kila mmoja wetu katika hatua fulani za maisha yetu huwa tunafikia sehemu ambayo kama vile tunataka kukata tamaa.Bila kujali tunafanya kazi ya kuajiriwa,tunajiajiri,tunafanya biashara,tunalima n,k kila mmoja watu kuna wakati huwa anapitia hali hii kwenye maisha yake.Ila kitu cha msingi ni kuwa ili uwe mmoja wa wachache ambao watafanikiwa kumaliza hadi mwisho wa mashindani ni lazima ufanye kiapo cha kumaliza ulichokusudia hadi pale utakapopata suluhisho bila kukata tama yoyote.

Moja ya mtu ambaye ameshawahi kunisisimua na kunipa hamasa ya kutafuta ninachokitaka na kuhakikisha kuwa nimekipata ni mwanariadha Read more

Ufanye Nini Unapojikuta Umefanya Kosa Kubwa Maishani

Moja ya tatizo kubwa sana linawalowakabili watu ni hali ya kushindwa kujisamehe baada ya kuwa wamefanya kosa fulani kubwa kwenye maisha yao.Kuna watu ambao wamekosa kujiamini tena katika maisha yao.Kuna watu wanajutia kuwa walichezea fura yao ya kusoma na leo imewasababishia wasiwe watu ambao wana elimu nzuri,kuna watu ambao waliwahi kupendwa sana ila wakapoteza hiyo fursa na leo wameshindwa kuupata ule upendo tena,kuna watu ambao waliwahi kupata pesa nyingi sana na wakazitumia vibaya na leo wako kwenye madeni ama wanaishi maisha magumu n.k
Kwenye maisha angalau kila mtu kuna siku aliwahi kufanya maamuzi fulani ama akachukua hatua fulani ambayo ilimletea majuto ya muda mrefu.Wakati wengine huwa wanaweza kujisamehe na kusonga mbele kuna wengine hali hii huwatesa maisha yao yote na huwasababisha kutokuishi maisha ya furaha na wanakosa hamasa ya Read more

Mambo 3 Ya Kujikumbusha Kila Siku Kama Unataka Kushinda Changamoto

Kila siku unakutana na watu na mazingira ambayo yatakuwa yanatishia sana mafanikio yako aktika kutimiza malengo uliyonayo kwenye maisha.Hii sio wewe tu peke yako,kila mtu ambaye anataka kufanikiwa katika  maisha huwa anakutana sana na hali hii.Kuna changamoto ambazo kila siku zitakuwa kama zinakuambia kuwa hauwezi tena kuendelea mbele hatua moja zaidi.Nimejifunza kuna mambo 3 ya kujikumbusha kila siku kama kweli unataka kubakia kwenye mstari: Read more