Navigate / search

Sabasaba – Kutoka siasa ni kilimo, hadi siasa ni biashara

Siku moja nilimuuliza mtu ninayemuheshimu na kumuamini sana swali;Hivi kwa nini siku ya wakulima ilihamishwa kutoka sabasaba hadi nanenane?Kwa nini wasingeanzisha siku mpya ya biashara iwe nane nane na sabasaba ikabaki ni maadhimisho ya kilimo?Ukweli ni kwamba alikosa jibu la kuniambia zaidi ya kusema ni uamuzi wa serikali.Ukweli ni kwamba hakuna sababu yoyote ya kihistoria ya tarehe 8 mwezi wa 8,bali siku ya tarehe 7 mwezi wa 7 ni siku muhimu sana katika historia ya nchi yetu.

Read more

Uchaguzi wa Afrika ya Kusini umetoa funzo kwa siasa za Tanzania

Wakati siku za uchaguzi zilivyokuwa zinazidi kukaribia nchini Afrika kusini watu wengi walikuwa na mtazamo kuwa Chama cha ANC(Afrika National Congress) na mgombea wake Jacob Zuma wangepata ugumu sana katika kushinda uchaguzi huo.Wachambuzi wengi waliokuwa wanauzungumzia uchaguzi huo walionyesha hofu kubwa kuwa ANC ingeshuka kwa asilimia kubwa katika kura zake na kupoteza nguvu yake kabisa katika bunge la nchi hiyo.Na dalili zilikuwa wazi kuwa Rais Zuma angekabiliwa na upinzani mkubwa,kuzomewa mara mbili katika msiba wa Mandela na wakati wa mechi ya soka kati ya Afrika kusini na Brazil zilituma ujumbe mchungu kuelekea uchaguzi huo.

Read more

Miaka 20 maadhimisho ya mauaji ya Kimbari Rwanda; Afrika bado haijajifunza?

Wanasiasa, vyombo vya habari na matumizi ya dini na ukabila yanaendeleza migogoro Afrika – Nimekumbuka ile kauli ya Rais ajaye Tanzania Hatatoka Kaskazini.

Mwezi huu yalianza maadhimisho ya kukumbuka mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda miaka 20 iliyopita(1994) ambayo yalishuhudia watu kati ya 800,000-1,000,000 wakipoteza maisha ndani ya siku mia moja kati ya April 7 na julai 15,1994.Ni mauaji ambayo hayakuwahi kutokea mahali popote katika kiwango kikubwa cha namna hii.Mauaji haya ya kutisha yaliwalenga zaidi watusi na wahutu ambao walikuwa na msimamo wa huruma kwa wahutu(moderate hutus).

Read more

Matumizi makubwa serikalini chanzo cha umaskini wa kujitakia

Ripoti ya IMF-Tanzania imethibitisha hilo

Mara tu baada ya nchi za Afrika kupata uhuru katika miaka ya 1960 zilijikita katika harakati kubwa za kujikwamua kutoka katika utegemezi wa uchumi kwa wageni.Juhudi hizi ziliendeshwa na kauli mbiu maarufu ya “Africanisation”-Madaraka kwa waafrika katika kila sekta.Hii ilifanyika bila kujali utaalamu uliokuwa unahitajika na ilisababisha viwanda vingi tulivyorithi toka kwa wakoloni kufa kwa kasi na nchi za afrika zilijikuta katika hali ngumu ya uchumi tena.Nchi nyingi ziligeukia kutafuta mikopo na misaada kutoka kwa wakoloni walewale ambao iliwafukuza hapo kabla.

Read more