Navigate / search

Aina 3 Za Marafiki Na Uhusiano Wao Na Mafanikio Yako

Marafiki zako wana nguvu ya kukufanya ufanikiwe ama kukufanya ushindwe kufanikiwa.Kuna watu wengi sana ambao wameshindwa kabisa kufikia katika kilele cha hatima zao kwa sababu tu wameendekeza kuwa na marafiki ambao wamekuwa kikwazo kwa maisha yao.Ila kuna wengine wameshindwa kabisa kufikia kilele cha mafanikio yao kwa kushindwa kutumia vizuri marafiki walionao.Siku zote kumbuka kuwa kila rafiki uliye naye lazima anakuathiri kwa namna fulani-Inawezekana akakuathiri kwa uzuri(Positive) ama akakuathiri kwa ubaya(Negative).Kwa sababu hii,ni lazima kila wakati uwe mtu ambaye unatathmini kuhusu maisha yako na wale wanaokuzunguka na jinsi wanavyochangia kukufanikisha ama kukukwamisha.Katika kitabu changu cha TIMIZA MALENGO YAKO Kwenye mbinu ya 30 nimeeleza mambo 4 ambayo unatakiwa
kuyafanya kuhusiana na kila rafiki uliyenaye ili kuhakikisha kuwa anakuwa msaada badala ya kuwa ni kikwazo kwenye maisha yako,hii inaitwa “Friendship Audit”.

Leo ningependa kuelezea aina za marafiki ambao unawahitaji katika maisha yako kila wakati kama kweli unataka kufanikiwa:
Aina ya kwanza tunawaita marafiki wa kukusukuma katika hatima yako(Destiny Pushers).Hawa ni aina ya marafiki ambao kila wakati watakuja katika maisha yako ili kuhakikisha kuwa hauishii njiani katika kutimiza kile ambacho umekusudia.Destiny Pushers ndio wale ambao mnaweza kupotezana lakini ukiwa katika wakati unataka kukata tamaa,uko chini sana kwenye maisha yako,wakati unaona giza nene-Hawa ndio wakati wao wa kukutia moyo na kukuambia kuwa unaweza.Aina hii ya marafiki huwa wanakuamini kwa kiwango kikubwa sana ambapo kuna wakati huwa unahisi kama vile wanakuamini kuliko wewe mwenyewe unavyojiamini.Ndio maana wakati wowote utakapoonyesha ulegeveu wa kutopiga hatua watakuwepo pale kukusisitiza kusogea mbele na kukuonyesha kuwa hata kama hakuna anayekuamini basi wao wanakuamini.Je,unamjua yeyote katika maisha yako ambaye ni rafiki wa namna hii?
Tatizo kubwa ambalo hutokea ni kuwa kwa sababu marafiki wa namna hii huwa wepesi sana kukusaidia na mara nyingi huwa hawalalamiki hata wewe usipowasaidia-Huwa ni rahisi kwanza kuwasahau lakini pia huwa tunawachukulia poa sana(We take them for granted).Leo jaribu kumkumbuka rafiki yeyote wa namna hii na mpigie simu,mtumie ujumbe wa simu,mnunulie zawadi n.k Fanya kitu chochote unachoweza kuonyesha shukrani zako kwake.
Aina ya pili ya marafiki ni wale ambao wanaitwa “Strategic Connectors”-Hawa huwa wanakuja kwa kusudi maalumu la kukusaidia kukuunganisha na fursa fulani ama na watu fulani tu kisha wanapotea.Mara nyingi marafiki wa namna hii huwa hawakai katika maisha yetu kwa muda mrefu sana kwani wanakuwa ni marafiki wa muda mfupi.Kosa kubwa ambalo watu wengi huwa wanalifanya katika maisha yao ni kujaribu kulazimisha marafiki wa namna hii waendelea kubakia katika maisha yao kwa muda mrefu zaidi ya inavyotakiwa.Ni lazima ukubaliane na ukweli huu kuwa kuna aina fulani za marafiki ambao hautaweza kudumu nao katika maisha yako,watakuja watafanya wema kisha wataondoka.Usijisikie vibaya wala usijaribu kuwan’gang’ania zaidi ya muda wao wanaotakiwa kukaa.Si lazima uwe umegombana nao,muda wao ukifika na wakifanikiwa kukuunganisha na fursa/mtu fulani huwa hawana hamu tena ya kuendeleza urafiki tena.
Aina ya tatu huwa tunaiita ni “Distractors”-Hawa kazi yao kubwa ni kuja kukupotezea mwelekeo wa maisha yako.Mara nyingi ukianza tu kujiruhusu kuwa karibu na marafiki wa namna hii utaanza kujikuta unajiingiza katika tabia ambazo sio sawa na unajikuta ule moto wa kujiletea maendeleo binafsi katika maisha yako unapotea kabisa.Hawa mara nyingi huwa wanaua ndoto ambazo watu huwa nazo,wanakuingiza katika vitu ambavyo baadaye vitakupa hasara na mara nyingi wakikushauri basi lazima ushari wao utakupelekea kuwa na majuto kwenye maisha yako.Uwe makini nao.Je,una rafiki yoyote ana sifa hii?Basi jitahidi kuweka umbali naye ama kupunguza mambo ambayo unamshirikisha katika maisha yako.
See You At The Top
@JoelNanauka

Leave a comment

name*

email* (not published)

website