Navigate / search

Adui Wa 7:Kukosa Utayari Wa Kuanza Upya

Adui wa mwisho katika mfululizo huu ambaye amewaangusha watu wengi sana ni ile hali ya kukata tamaa kuanza upya katika maisha yako.Kila mmoja wetu kuna siku na nyakati ambazo anaweza kuzipitia ambazo zinaweza kuonyesha kama vile hakuna tena tumaini la kufanikiwa tena ama kuwa na furaha tena ni kama vile mazingira na hali zote ambazo zinakuzunguka zitaonyesha kuwa hauwezi kuinuka tena,hauwezi kufanikiwa katika ndoot yako,hauwezi kuwa na furaha tena,hauwezi kupiga hatua tena.

Kuna watu ambao walishawahi kupata hasara ya biashara na wanaona haiwezekani kufanikiwa tena,kuna watu walishawahi kuumizwa katika mahusiano na wanaona kama vile hawawezi kupenda ama kupendwa tena,kuna watu walishawahi kusoma kwa bidii na wakafeli na wameshaona ni kama vile hawawezi kufaulu tena.

Usikubali jambo lolote katika maisha yako likuambie kuwa haiwezekani tena;Kila mtu ana fursa ya kuanza upya.Kila mtu ana uwezo wa kuinuka na kusonga mbele.Waldo Emerson alisema,mafanikio yetu makubwa hayaji kwa sababu hatujawahi kuanguka bali yanakuja kwa sababu kila tukianguka huwa tunajitahidi kuinuka tena.Bila kujali ni kitu gani kimekusababishia maumivu,kitu gani kilikuangusha,kitu gani kimekutoa machozi-Unayo fursa ya kuanza upya katika maisha yako.Ningependa kukushauri usikilize CD yangu inayofundisha mambo 4 ambayo yanaleta mafanikio yasiyojulikana na wengi na ile ya mambo 7 ambayo usipoyajua utabakia kuwa maskini maisha yako yote.

Kama ungependa kupata mafundisho ya namna hii kila siku basi unaweza kutembelea na kulike ukurasa wangu wa facebook(Joel Nanauka) au instagram (joel_nanauka) na utapata mafundisho ya kukusaidia kuifanikisha ndoto yako kila siku.Pia unaweza kujiunga na madarasa kwa njia ya WATSAPP kwa kutuma neno “NDOTO YANGU” ikifuatiwa na jina lako kamili kwenda 0655 720197 na utaunganishwa na hakuna gharama yoyote ile utakayotozwa.

Kama ungependa kupata ushauri zaidi kuhusu namna ya kutimiza malengo yako ama ungependa kunieleza Makala hii ilivyokusaidia,tafadhali tuwasiliane kwa barua pepe(jnanauka@gmail.com ama kwa simu 0743 868507 au tembelea tovuti yangu www.JoelNanauka.Com).

See You At The Top

Joel Nanauka

Life Coach&Public Speaker

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website