Navigate / search

Adui Wa 6:Kushindwa Kufanya Mambo Kwa Ubora

 

Kijana mmoja aliyekuwa ni fundi wa nyumba maarufu sana alifanya kazi katika kampuni kwa muda mrefu sana kwa bidii.Baada ya kuona anakaribia kustaafu na hakuna dalili ya yeye kupandishwa cheo wakati wowote,alianza kuwa mzembe wa kazi.Basi zikiwa zimebakia siku chache sana kabla ya muda wake wa kustaafu alipewa kazi nyingine ngumu sana ya kujenga nyumba nzuri ya kisasa.Bosi wake akamwambia kuwa aisimamie na achague anataka kuipendezesha kwa vitu gani,aiwekee swimiing pool bora kabisa na atumie malighafi zozote ambazo anazitaka katika ujenzi.Kwa kuwa alikuwa anajua muda wake wa kustaafu umeshafika na hakuna dalili ya yeye kupanda cheo tena,aliifanya kazi ile kwa uzembe wa hali ya huu sana,alitumia malighafi dhaifu na hakutumia ubunifu katika kuipendezesha.

Baada ya kukamilisha ujenzi alimpa taarua bosi wake.Bosi wake alifurahi sana na kumpongeza kwa kuwa mtu ambaye amekuwa mfanyakazi mwaminifu kwa muda mrefu wa katika kampuni ile.Baada ya kuwa amebakiza mwezi mmoja wa kustaafu kaziyake,bosi wake alitoa taarifa kuwa ameandaa tafrija ya kumuaga kwa heshima kutokana na kazi aliyofanya kwa uaminifu.Ukweli ni kuwa hakuwa na furaha na wala hakushtushwa na taarifa hii kwani hitaji lake kubwa halikuwa hilo.Alianza kuwaambia maneno wafanyakazi wenzake kuwa “Baada ya kunipa pesa au kuniongezea mshahara kipindi chote hiki,anajifanya mwema sana kuniandalia sherehe wakati ndio nastaafu.”.Kama ilivyo ada wafanyakazi wenzake wengi walimuonea huruma na kukubaliana na maneno yake.

Bosi alitangaza kuwa kwa sababu amefanikiwa kujenga nyumba yake ya mwisho basi sherehe ya kumuaga ifanyike katika bustani ya nyumba ya mwisho ambayo aliijenga.Siku ya tukio ilipofika na muda wa bosi wake ulipofika wa kuongea,alisema kwa kifupi-“Nakuhsukuru sana kwa kuwa mfanyakazi mwaminifu miaka yote tumekuwa pamoja,naomba nikukabidhi ufunguo wa nyumba hii kwani ni zawadi yako”.Akiwa ametokwa na macho alianza kulia sana,wengi walifikiri ni kilio cha furaha kwa kupewa zawadi,lakini haswaa kilikuwa ni kilio cha majuto kwa kutotumia ubor akwa nyumba ambayo hakujua kama ni yak wake.

Mara nyingi fursa tulizonazo kwa sasa ndizo ambazo hutengeneza fursa kubwa ambazo tunazitamani.Bila kujali leo unafanya nini katika maisha yako,bila kujali unalipwa kiwango gani,jifunze kufanya vitu kwa viwango vya hali ya juu kwani kwa njia hiyo utakuwa unatengeneza fursa ya kupata fursa kubwa zaidi.Hebu jikague katika majukumu yako ya leo unafanya kazi kwa bidii na kwa ubora kiasi gani?

Moja ya msemo huwa napenda sana kuwaambia watu ni “Ubora ndio alama kubwa ya watu ambao wanakuwa wakuu katika maisha yao”(Excellence is the Mark of Greatness).Njia mojawapo ya kujipima kama utafika mbali sana ni pale ambapo kila wakati kazi zako huwa zinalalamikiwa kwa ubora.

Jijengee sifa ya kufanya mambo kwa ubora kiasi ambacho kama umeajiriwa basi bosi wako atakuta makosa machache sana katika kazi ambazo anakupatia na haitamlazimu kutumia muda mwingi.Ifike mahali hadi wawe wanasema-“Kama kazi hii imefanywa namtu fulani basi sina wasiwasi nayo”.

Kufanya biashara yako kwa ubora inamaanisha kuwahudumia wateja wako kwa kiwango ambacho watakuona kuwa hauna mpinzani katika kile ambacho unakifanya.Siku zote kumbuka kuwa unapofanya kwa ubora kwa mtu mmoja huwa inakufungulia milango mingine mingi ambayo itakusogeza hatua kubwa zaidi.

Hata hivyo jambo lingine la kujua ni kuwa unapofanya kwa ubora wajibu ambao uko katika mikono yako huwa inakuongezea hali ya kujithamini na kujikubali(Self-esteem).Hiki ni kitu muhimu sana kwenye maisha yako kwani huwa inapelekea kukujengea ujasiri wa hali ya juu katika eneo lako.Ukiwa mtu ambaye kila wakati watu wengine huwa wanakosoa ubora wa kile unachokifanya,basi unaweza kujikuta unapoteza hali ya kujiamini katika maisha yako.

Leo amua kuanza kujitengenezea sifa ya kufanya mambo kwa ubora kiwango ambacho watu wakitaka kufanya kitu katika “field yako” wawe wanaambiana kuwa,ukitaka kupata kwa ubora wa hali ya juu basi mtafute(jina lako).Unaweza kununua kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO ukasoma kwenye sura ya sifa za watu wanaotimiza malengo yao na ukajifunza mbinu wanazotumia kujenga ubora wa mambo ambayo wanayafanya kwenye maisha yao.

See You At The Top

#TIMIZAMALENGO

 

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website