Navigate / search

Adui Wa 5 Kukosa Nidhamu

Watu wengi sana wana vipaji,wana fursa na wana elimu pia lakini kwa sababu ya kukosa nidhamu katika maisha yao wameshidnwa kupiga hatua inavyotakiwa.Nidhamu maana yake ni kufanya kitu ambacho unajua kuwa ni muhimu kwa wakati huo kukifanya aidha unapenda ama la.Nidhamu maana yake hauishi kwa kufanya kinachokupa raha bali unaishi kwa kufanya kilicho muhimu (You don’t live by Convinience but you live by Necessity).

Mtu ambaye hana fursa nyingi lakini ana nidhamu atamshidna mtu ambaye ana fursa nyingi ila hana nidhamu.Mtu ambaye ana kipaji cha kawaida ila ana nidhamu kubwa siku zote atamshinda mtu ambaye ana kipaji kikubwa ila hana nidhamu kabisa.Kuwa na nidhamu maana yake ni kufanya kile ambacho ulidhamiria kufanya hata kama haujisikii kufanya.

Watu wengi sana huwa wana malengo makubwa na mara nyingi wana dhamira ya kufanya mambo mengi,ila baada ya muda wanashangaa kuwa ile munkari ya kufanya imepotea kabisa.Hata wewe hebu jaribu kujichunguza;ni mambo mangapi ambayo ulidhamiria kuyafanya na sasa umefika wakati imeshindikana haufanyi tena?

Kuna maeneo matatu ambayo unaweza kuonyesha kiwango chako cha nidhamu.

Eneo la kwanza ni kwenye matumizi ya muda wako.Dalili ya kwanza kuwa haun nidhamu na muda ni pale ambapo utajikuta huwa hauna mpangilio wa siku yako.Kwa ufupi ni kuwa,unafanya mambo kadiri yanavyojitokeza katika siku yako lakini hakuna wakati unakaa na kuipanga siku yako iweje.

Ushauri wangu ni kuwa jaribu kila siku kuwa na orodha ya vitu ambavyo uantakiwa kuvikamilisha na hakikisha unavisimamia na kuvifanya bila kukosa.Watu ambao hawana nidhamu ya muda hufikiria kuwa wana muda mwingi sana duniani na wanakuwa na tabia kughairisha mambo kila wakati na matokeo yake huwa wanakuja kujialumu wakishakuwa wazee.

Watu ambao hawana nidhamu ya muda ndio wale ambao wakiwa wameajiriwa huwa wana bidii ya kuamka mapema lakini siku wakijiajiri wenyewe huwa wanaamka muda ambao wanataka wenyewe.Watu wasio na nidhamu ya muda huwa hawajisikii vibaya kuchelewa ama kuchelewesha.Siku zote kumbuka kuwa namna unavyothamini muda ni dalili inayotosha kuwafanya watu wakuchukulie kama mtu makini ama le kwenye maisha yako.Kuna watu ambao hawajali muda hadi wanajulikana na kila mtu anayewazunguka.

Kumbuka kuwa muda ndio rasilimali pekee ambayo ukishaipoteza hautaweza kuipata tena.Kila unapopoteza muda wako unapoteza sehemu ya maisha yako.Ili kujua hilo kila wakati jiulize-“Hivi hiki ninachofanya ndio matumizi bora ya muda wangu?”.Wakati wowote ambao utagundua kuwa unachofanya sio matumizi mazuri ya muda wako basi hakikisha unakiacha na unafanya kitu kingine.

 

Eneo la pili ambalo unatakiwa kuonyesha nidhamu ni eneo la matumizi ya fedha zako.Umaskini sio matokeo ya kuwa na kipato kidogo bali ni matokeo ya kutokuwa na mpango mzuri wa matumizi ya kile kidogo ulichonacho.Siku zote usisahau kuwa kila pesa unayopata leo bila kujali ni kidogo kiasi gani,ni mbegu ya kukusaidia kesho yako.Kama hauwezi kutumia vizuri kidogo ulichonacho leo basi ujue hautaweza kutumia vizuri kikubwa kitakapokuja mikononi mwako.

Watu wengi huwa wanajua wanaingiza kiasi gani kwa mwezi lakini wapo wengi sana huwa hawajui wanatumia kiasi gani kwa kila mwezi katika maeneo tofautitofauti.Kama wewe hauna bajeti ya matumizi yako kwa kila mwezi,hiyo inamaanisha kuwa umekosa nidhamu ya pesa ambayo itakuwa ni chanzo chako cha umaskini.Unajua kwa mwezi huwa unanunua muda wa maongezi kiasi gani?Huwa unatumia mafuta ya kiasi gani?Huwa unatoa sadaka kiasi gani?Huwa unatoa michango/kusaidia watu kwa kiasi gani?Lazima kwenye kila eneo ujenge kiasi maalumu unachofanya.

Eneo la tatu ambalo unahitaji kuwa na nidhamu ni eneo la kufanya mambo uyliyoamua.Hii ina maanisha kuwa kama umeamua kufanya jambo fulani basi usiwe mtu wa kughairisha ghairisha kila wakati.Ukiamua kuchukua hatua fulani maishani mwako basi uwe na nidhamu ya kufanya.Hebu fikiria tangu mwaka huu uanze uliamua kufanya mambo mangapi na ni mangapi ambayo umeshafanya na ni mangapi ambayo umeghairisha?Kukosa nidhamu ya kufanya mambo kama ulivyodhamiria ni aduui mbaya wa mafanikio yako.Ulisema utaanza kuweka akiba,ulisema utaanza kufanya mazoezi,ulisena utaanza kusoma vitabu,ulisema utaanza kufanya biashara-Mbona uanendelea kughairisha?Ili kujua mbinu za kuishinda tabia ya kughairisha mambo,uanweza kutafuta kitabu changu cha ISHINDE TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO kwa bei ya 5,000/- kupitia 0655 094 875.

Nitashukuru kama utanisaidia kushare ujumbe huu na marafiki zetu wengine ili wamshinde adui huyu.

@JoelNanauka

See You At The Top

#TIMIZAMALENGOYAKO

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website