Navigate / search

ADUI WA 4: Kukosa Maarifa Yanayotakiwa

Siku zote kiwango cha mafanikio yako kinatokana na kiwango cha maarifa uliyonayo juu ya jambo unalolifanya.Kuwa na malengo na bidii peke yake haitoshi juu ya kile unachofanya,ni lazima ujikite kuwa na maarifa ya kiwango cha juu sana katika kile unachofanya.Itashanagza sana kama wewe unataka kuwa mfanyabishara mkubwa sana lakini kila siku kazi yako ni kusoma magazeti ya udaku tu ama ni kuangalia novie tu.Kama unataka kuwa mfanyabishara mkubwa ni lazima ujikite katika kutafuta elimu na maarifa yahusuyo biashara,tafuta historia za wafanyabiashara waliofanikiwa usome historia zao,ujue vikwazo walivyokutana navyo,ujue mbinu walizotumia kufanikiwa na kukuza makampuni yao.

Kama wewe unataka kuwa mhubiri mkubwa ni lazima usome vitabu vinavyoeleza juu ya mafanikio ya wahubiri waliotangulia,ni lazima ujifunze makosa waliyofanya ili wewe usikosee katika maeneo hayohayo pia.Lakini itashangaza kama wewe unataka kufanikiwa kama mwanasheria mkubwa lakini kazi yako ni kusoma na kujadilia kuhusu maisha ya wanamuziki na wanamichezo tu kutwa kucha na hauna muda kabisa wa kuongeza maarifa kwenye eneo lako.

 

Hivi kweli unasema wewe unataka kuwa mkulima lakini hadi leo haujafanya juhudi ya kujifunza jambo lolote kuhusu kilimo?Kweli uko serious na unachotaka kukifanya?

Ili uwe bora katika kile ambacho umeamua katika maisha yako,fanya maamuzi ya kuwa na maarifa ya kiwango cha juu sana kuliko mtu wa kawaida katika eneo hilo.Hakikisha kuwa HAKUNA SIKU YOYOTE inapita katika maisha yako bila kujifunza kitu kipya katika eneo husika Kuna njia mbili uanweza kuzitumia kuongeza uwezo wako wa maarifa katika eneo ambalo unalifanya.

 

la maisha yako.Kwa wastani kila siku uantakiwa kusoma angalau kurasa kumi za kitu kuhusiana na taalamu ama shughuli unayotaka kuifanya.

Moja ni kuwa msomaji mzuri wa vitabu vinavyohusiana na eneo lako.Kuna watu mara ya mwisho wamesoma kuhusu taaluma yao si siku moja kabla hawajafanya mtihani wa mwisho.Baada ya hapo hawajawahi kusoma tena.Mabadiliko ya maarifa katika ulimwengu wa sasa yanaenda kwa kasi sana na inahitajika mtu ambaye kila wakati anapata maarifa mapya ili asipitwe na wakati.

 

Moja ya kauli muhimu sana ambayo aliwahi kuisema tajiri mkubwa Hernry Ford ni kuwa-“Bila kujali kama una miaka 20 ama 80 unapoacha kujisomea basi wewe ni mzee”

Kuna watu wengi sana kwa umri wao wa kuzaliwa ni vijana lakini ubongo wao umechakaa kama wazee wa miaka mingi.Kumbuka kuwa ubongo wako unahitaji kulishwa kama unavyoulisha mwili wako.Unahitaji kuwekeza kununua vitabu,kusikiliza masomo kwenye YouTube na kujisomea kupitia tovuti mbalimbali.Kuna watu wanasema hawana pesa ya kununua kitabu lakini kila mwezi wananunua nguo mpya,kuna watu wanasema hawana muda wa kusoma vitabu lakini kila siku wanapata muda wa kuperuzi mitandao,kusoma magazeti au kuangalia TV ama kukesha kuangalia series za movies.Jaribu kujiangalia na ujiulize “hivi MIMI ni KIJANA kwa NJE ila MZEE kwenye UBONGO?”.Tusije tukawa tunakuita kijana kumbe mwenzetu ulishazeka siku nyingi sana.

 

Njia ya pili ni kuhudhuria mafunzo mbalimbali ili kuongeza kiwango chako cha ufahamu.Kama ambavyo watu wanaweza kulipia pesa kwenda kwenye matamasha ya muziki kama fiesta ili kuburudisha nafsi zao na kutimiza matakwa ya hisia zao.Vivyo hivyo na wewe unatakiwa kutengeneza mazingira ya kuhakikisha kuwa unapata muda wa kwenda mahali ambapo maarifa ambayo yatakusaidia kupiga hatua huwa yanatolewa.Wakati mwingine daraja la hap ulipo na kule ambako unataka kwenda tofauti yake ni maarifa ya siku moja ambayo ukiamua kuyatafuta kuna siku utakutana nao.Watu wengi sana huwa wanapoelezea maisha yao huwa wanataja siku moja maalumu ambayo walipata maarifa ya kuwasaidia.Usichoke kutafauta maarifa.

 

Ukiona hasara kulipia gharama za kupata maarifa ya kukuvusha leo,utajikuta unapata hasara ya kutofanikiwa kesho.Jiwekee utaratibu kila baada ya muda fulani unahudhuria kozi ama mafunzo fulani ya kukusaidia kuongeza ufanisi.Hakuna kitu kibaya kama kuwa na shauku ya kufanikiwa lakini hauna maarifa yanayotakiwa ili ufanikiwe.Watu wengi sana wameishia kupata hasara,kuwachukia wengine kwa wivu na kuishia kwenye msongo wa mawazo kwa sababu usipokuwa na maarifa ya kutosha unajikuta unatumia nguvu NYINGI na unapata MATOKEO MACHACHE.

 

Panga mpango mzuri wa namna utakavyoongeza maarifa kuanzia leo.

Nafurahi kuwa nimetumia muda mwingi kuandaa ujumbe huu ili ukufikie,unaonaje nawe utumie sekunde moja kushare na mtu mwingine?Ahsante kwa kufanya hivyo.

 

@JoelNanauka

See You At The top

#TIMIZAMALENGOYAKO

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website