Navigate / search

ADUI WA 3-MAADUI 7 AMBAO LAZIMA UWASHINDE ILI UFANIKIWE

3.Hali ya kukosa mwendelezo katika kufanya mambo(Inconsistency)

Watu wengi mara nyingi sana hufikiri kuwa mafanikio ni matokeo ya kufanya jambo fulani kubwa mara moja na likabadilisha maisha yako.Lakini tafiti zote za mafanikio zimeonyesha kuwa mafanikio mar azote ni matokeo ya mambo madogomadogo ambayo huwa unayafanya kila siku.Kama unataka kubadilisha maisha yako hivyo ni lazima ubadilishe mambo ambayo huwa unayafanya kila siku katika maisha yako.

Brian Tracy aliwahi kusema-“Uwezo wako wa kuwa na nidhamu ya kuweka malengo mahsusi na kisha kila siku ukayafanyia kazi kidogokidogo ndicho kitu kinachoweza kukuhakikishia mafanikio kuliko kitu kingine chochote katika maisha yako.(“Your ability to discipline yourself to set clear goals, and then to work toward them every day, will do more to guarantee your success than any other single factor”).

Ili ufanikiwe ni lazima uwe matu ambaye unafanya mambo kwa mwendelezo unaotakiwa hadi umeona matokeo ambayo uanyatafuta.Katika kitabu chake cha the compound effect,Darren Hardy anazungumzia kanuni ya nguvu ya mwendelezo katika ukurasa wa 113 anaposema kama wewe na mimi wote tukichukua ndege kutoka Los Angeles hadi Mahattan,ila wewe ukiwa unatua kwenye kila mji ulioko njiani na mimi nikaenda moja kwa moja bila kusimama,hata kama kasi yako itakuwa maili 500 kwa saa na mimi nitaenda kwa maili 200 kwa saa bado nitafika mapema sana kabla yako (“If you and I flew planes from Los Angeles to Manhattan, but you took off and landed in every state in between, while I flew straight through, even if you went five hundred miles per hour in the air and I only traveled at a rate of two hundred miles per hours, I’d still beat you by a big margin”)

Kwenye maisha kasi peke yake haitoshi,unahitaji kuwa na mwendelezo wa kile unachofanya.Kuna watu wengi sana ambao wanafeli katika maisha sio kwa sababu hawafanyi bali huwa wanafanya kwa “kudononoa donoa”.Hawa ni wale watu ambao leo wanafanya kisha wanakaa mwezi mmoja kabla hawajafanya tena.Hawa ni aina ile ya watu ambao kila siku huwa wanaanza kitu kipya katika maisha yao,kiufupi ni kuwa huwa hawafanyi jambo moja kwa muda mrefu likakamilika.Wakianza kusoma kitabu basi wataishia njiani,wakianza kufanya biashara fulani basi kabla hawajafanikiwa utakuta wameshaanza biashara nyingine.

Ili ufanikiwe ni lazima uwe mtu ambaye uko unaweka nguvu kubwa katika kufanya jambo ulilochagua kulitimiza na uhakikishe kuwa kunalifanya kila siku bila kuachaacha njiani.Napenda sana msemo ambao Gretchen Rubin waliowahi kuusema kuwa nianchofanya kila siku kina faida kubwa kuliko ninachofanya mara moja moja.“What I do every day matters more than what I do once in a while.”

Ni kitu gani umeamua kuikifanya katika maisha yako?Umeamua kuwa nani katika maisha yako?Siri ya mafanikio yako haiko kwenye kusubiri kufanya jambo kubwa moja baada ya muda mrefu litakalokufanikisha bali siri ya mafanikio yako iko kwenye kuamua kufanyia kazi kila siku malengo ambayo umejiwekea bila kuchoka.

Kuanzia leo jiwekee ratiba ya kufanya mambo fulani kila siku ambayo yatakusaidia kuelekea katika mafanikio yako.Achana kabisa na tabia ya kufanya mambo kwa kudonoa dona katika maisha yako.Chochote ambacho umeamua kukifanya basi kifanye kwa mwendelezo kuanzia leo,usiwe mtu wa kuuishia njiani kila wakati.

Leave a comment

name*

email* (not published)

website