Navigate / search

ADUI WA 2-MAADUI 7 AMBAO LAZIMA UWASHINDE ILI UFANIKIWE

 

Concept of businessman choosing the right door

2.Kushindwa/Kuchelewa kufanya Maamuzi(lack/delay of decision making)

Mark Twain alisema miaka 20 kuanzia leo utajilaumu zaidi kwa mambo ambayo haukuyafanya kuliko yale ambayo uliyafanya (Twenty years from now you will be more disappointed by the things you didn’t do than by the ones you did do).Mara nyingi sana fursa ambazo zinaweza kubadilisha maisha yetu kwa kiwango kikubwa ni zile ambazo zinatuhitaji tufanye maamuzi bila kuchelewa na tuyasimamie maamuzi hayo.

Watu wengi sana wamefeli katika maisha yao kwa sababu ya kushindwa kufanya maamuzi kuhusiana na mambo muhimu wanayoyataka ama wasiyoyataka.Siku zote kumbuka kuwa hakuna kitu kinachoweza kutokea kwenyemaisha yako bila kwanza kufanya maamuzi.Kila unayemuona ni tajiri leo kuna siku aliamua kuachana na umaskini,kila unayemuona anafaulu mitihani leo kuna siku alichukia kufeli na akaamua kuanza kufaulu,kila uanyemuona ana  furaha leo kuna siku alifanya maamuzi na kuachana na vitu vilivyokuwa vinampa huzuni.

Hakuna mafanikio yanayokuja bila wewe mwenyewe kufanya maamuzi.Hapo ulipo leo na hivyo ulivyo,hautaweza kubadilika kama hautafanya maamuzi.Hivi utaendelea kulalamika hadi lini,utaendelea kuteseka hadi lini,utaendelea kufanya kitu usichokipenda hadi lini?Kumbuka kuwa kuna baadhi ya mambo mtu mwingine anaweza kukuamulia lakini kuna mambo ambayo ni wewe mwenyewe ndio uanweza kuamua.Leo hebu chunguza maisha yako na ujiulize,kuna maamuzi gani ambayo natakiwa kuyafanya ili kubadilisha maisha yangu?

Watu wengi huogopa kufanya maamuzi kwa sababu mbalimbali.

Moja ni wale wanaoogopa kufanya maamuzi kwa sababu ya kuogopa watu watasemaje.Kama wewe ni mtu ambaye kila wakati unaogopa watu watasemaje kuhusu maamuzi yako basi hauwezi kufanikiwa kwa haraka katika maisha yako.Kumbuka kuwa kwenye kila maamuzi ya maana ambayo yanahusu mafanikio yako ni lazima kuna watu itabidi uachane nao,au wasiyafurahie ama watakutenga kabisa.Hii ndio maana Aristotle alisema kama hupendi kukosolewa basi-Usifanye kitu chochote,usiseme kitu chochote na usiwe mtu wa maana(To avoid criticism say nothing, do nothing, be nothing).Inawezekana hata unaposoma Makala hii leo kuna maamuzi mengi sana ambayo umeshindwa kuyafanya katika maisha yako kwa sababu unawaza watu watasemaje ama itakuwaje.

Kanuni ya Daniel amen ya 18/40./60 imewasaidia watu wengi sana kuanza kuishi maisha ya mafanikio  kuachana na ile hali ya kuogopa kufanya maamuzi.Kanuni hii inasema:Mtu anpokuwa na miaka 18 huwa anawaza kila wakati watu wanafikiri nini juu yake,akifikisha miaka 40 huwa hajali tena watu wanasema nini lakini akifikisha miaka 60 anagundua kuwa miaka yote hiyo hakuna mtu alikuwa anamfikria yeye kila mtu alikuwa anajiwazia mwenyewe.(When you’re 18, you worry about what everybody is thinking of you; when you 40, you don’t give a damn what anybody thinks of you; when you’re 60, you realize nobody’s been thinking about you at all).Kuna mambo mengi sana ambayo inawezekana unayawaza kila wakati ukiamua watu watasemaje lakini ukaja kushangaa hakuna ambaye hata anawaza kuhusu hilo.

Pili watu huwa hawachukui maamuzi kwa sababu wanaogopa kufeli katika maisha yao,Kuna mtu mmoja aliwahi kusema kuwa watu wengi wako tayari kuiishi jehanam wanayoijua kuliko kujihatarisha kuanza safari ya kwenda mbingu wasioijua(People prefer a known hell to an unknown heaven because it is familiar).Watu wengi sana hawafanyi maamuzi katika maisha yao kwa sababu wako tayari kuishi katika maisha magumu na wasiyoyapenda lakini wameyazoea kuliko kujaribu kufanya mambo ambayo hawayajazoea lakini yanaweza kubadilisha maisha yao.Kuna watu wako kwenye kazi ambazo ukweli hawazipendi kabisa lakini lakini kuliko wafanye maamuzi magumu wanaona bora waendelee kuishi katika magumu waliyoyazoea kuliko kujaribu kutafuta mazuri wasiyojua.

Sina uhakika na maisha unayoishi leo unayafurahia kiasi gani na uko tayari kuendelea kuwa katika hali hiyo kwa muda gani?Ili utoke hapo ulipo kwenda unakotaka ni lazima ufanye maamuzi bila kuchelewa.Hebu jiulize-“Hivi nitaishi hivi hadi lini?”,”Hivi nitakuwa katika hali ya huzuni hadi lini?”,”Hivi nitaendelea kufeli hadi lini?”,Hivi nitaendelea kulia hadi lini?”,Hivi nitaendelea kumlaumu na kumchukia mtu fulani hadi lini?”

Hatua ya kwanza ya kubadilisha maisha yako ya sasa ni kufanya maamuzi bia kuchelewa-Kuna mambo katika maisha yako yanaweza kubadilika kwa kusubiri muda mrefu upite na yanabadilika yenyewe lakini kuna maamuzi katika maisha yako hayawezi kubadilika hadi wewe mwenyewe ufanye maamuzi.Leo ifanye kuwa ni siku ya maamuzi muhimu katika maisha yako,usikubali kuendelea na maisha unayoishi sasa hivi.Fanya maamuzi kuhusiana na mahusiano yako,fanya maamuzi kuhusiana na kazi yako fanya maamuzi kuhusiana na biashara yako,fanya maamuzi kuhusiana na kesho yako.

Kumbuka kuwa kadiri unavyofanya maamuzi yako haraka ndivyo unavyoongeza uwezekano wa mafanikio yako kwa haraka.

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website