Navigate / search

ADUI WA 1-MAADUI 7 AMBAO LAZIMA UWASHINDE ILI UFANIKIWE

MAADUI 7 AMBAO LAZIMA UWASHINDE ILI UFANIKIWE

Moja kati ya misemo Maarufu sana katika bara la Afrika ni ule unaosema,kama hakuna adui aliye ndani yetu basi hakuna adui yeyote wa nje ambaye anaweza kutudhuru kwa namna yoyote ile(If there is no enemy within, the enemy outside can do us no harm).Huu ndio ukweli ambao hauwezi kufichika au kupingwa,kama ukishinda ndani ya moyo wako na kuamini kuwa aweza kufanikiwa basi hakuna kitu/mtu yoyote yule ambaye anaweza kukusababisha usifanikiwe katika maisha yako.

Katika sekta ya mafanikio kuna vitu vingi sana ambavyo kila wakati vitakuwa vinajaribu kuzuia ama kupunguza kasi yako ya mafanikio.Hata hivyo katika utafiti wangu nimegundua kuwa kuna maadui 7 ambao kila aliyefanikiwa aliwashinda na hivyo kila ambaye anataka kufanikiwa ni lazima awafahamu na awashinde maadui hawa.Ukweli ni kuwa mafanikio si jambo rahisi kabisa na hii ndio sababu kuwa waliofanikiwa ni wachache sana.Ili nawe ujiunge na hao wachache ni lazima ufanye bidi kuwashinda maadui hawa.

Unapomuona mtu amekata tamaa na ameshindwa kuendelea kuifutailia ndoto ya maisha yake,jua kwamba maadui hawa wamemhsinda,unapomuona mtu amekata tamaa na ameamua kuishi maisha ya umaskini ujue maadui hawa wamemshinda,ukisikia mtu anasema haiwezekani kufanikiwa kwenye maisha tena ujue maadui hawa wamemshinda,ukisikia mtu anawalaumu wengine kwa maisha magumu aliyonayo,ujue maadui hawa wamemshinda.

Ukikutana na mwanamuziki mkubwa aliyefanikiwa basi ujue amefanikiwa kuwashinda maadui hawa,ukikutana na mtu aliyefanikwia katika biashara yake ujue amewashinda maadui hawa,ukikutana na mtu amepanda cheo na ni bosi mkubwa sana,ujue amewashinda maadui hawa.

Je nawe unataka kufanikiwa?Je nawe unataka kutimiza ndoto yako?Kuna jambo ambalo ungependa kulifanikisha mwaka huu?Kuna jambo ungependa kulifanikishab kabla haujaondoka duniani?.Kama jibu lako ni ndio kwa maswali haya basi ni vizuri ukawafahamu maadui hawa na ukajua namna ya kuwakabili kuanzia leo ili wasikuzuie mafanikio yako.Kitu cha ajabu ni kuwa hata kama wengine wote umewashina basi adui mmoja tu anayo nguvu ya kukufanya usifanikiwe,hivyo ni lazima ujipange kuwashinda maadui wote bila kuchoka.Maadui hao ni hawa wafuatao:

  1. Kukosa Malengo Thabiti(Lack of Clear Goals)

Adui wa Kwanza:Kukosa Malengo Mahsusi

Mtu ambaye ana uwezo mdogo/hana kipaji lakini akawa na malengo thabiti,siku zote atafanikiwa zaidi ya yule mwenye uwezo mkubwa na vipaji lakini hana malengo thabiti katika maisha yake.Watu wengi wamefeli katika masiha sio kwa sababu hawana uwezo ama hawana fursa bali kwa sababu tu wamekosa kuwa na malengo katika maisha yao.Maisha bila malengo ni sawa na kuwa na gari lisilo na dereva ndani,linaweza likaanza safari bali halitakuwa na uwezo wa kufika linakoenda.

Watu wengi wako bize,huwa wanaamka asubuhi na mapema,wanajishughulisha kufanya mamabo mbalimbali na ukweli ni kuwa wana bidi lakini ukiangalia maisha yao,hayafanani kabisa na juhudi zao.Kumbuka kuwa kuwa na bidi na kutumia nguvu kufanya mambo bila malengo ni kupoteza muda.Ni lazima ujiulize,hivi lengo langu ni kuwa nani?Lengo langu ni kufanikiwa katika jambo lipi?Lengo langu ni kufika wapi?.Siku zote kwenye maisha wale wasiokuwa na malengo huwa ni watumwa wa wale wenye malengo.Ningependa kujua katika maisha yako uanyo malengo?Kama bado hauna basi leo hakikisha unatengeneza malengo ya maisha yako.Weka malengo yako yam waka huu,weka malengo yako ya miaka 5 na weka malengo yako ya muda mrefu.Malengo haya yasibakie kichwani wkako tu,yaandike katika adftari ama mahali ambapo utakuwa unayapitia kila wakati na kujikumbusha.

Kwa kila lengo unalojiwekea basi jitahidi liwe mahsusi sana.Huwa ninapofundisha katika semina zangu nawaambia watu kuandika malengo yako katika namna kama vile wanatoa oda ya kwenda kutengenezewa nguo(kwa kawaida utachagua rangi ya kitambaa,vipimo vya urefu,kiuno ufupi,mtindo n.k).Vivyo hivyo malengo yako yanatakiwa yawekwe kwa vipengele vyote.Kwa mfano usiseme nataka kuongeza kpato mwaka huu,bali sema-Nataka kuongeza kipato changu wka shilingi 300,000 kila mwezi itakapofika mwezi wa kumi na moja.Usiseme nataka kupunguza uzito,hapana-Sema nataka kupunguza uzito kwa kilo 7 ifikapo tareh 25 desemba,2016.Usiseme mwaka huu nitaongeza elimu-Sema mwaka huu nitajiunga na chuo fulani(unakitaja) tareh 10 oktoba ili kuanza kusoma kozi ya udereva.Kdiir malengo yako yanavyokuwa mahsusi na umeyaandika basi ndivyo uwezekano wa kufanikiwa unavyoongezeka.

Hebu jichunguze?Umeshawahi kuwa na malengo thabiti yaliyoandikwa katika maisha yako?.Takwimu zinaonyesha kuwa watu wenye malengo thabiti hufanikiwa mara kumi zaiid ya watu wasio na malengo thabiti.Jiunge na watu wanaofanikwia sana kwa kuwa na malengo thabiti leo.

 

Leave a comment

name*

email* (not published)

website