Navigate / search

Jinsi Ya Kujenga Msingi Wa Mafanikio

Siku moja mwandishi mmoja wa habari alikuwa akimhoji Muhamadi Ali,bingwa wa ngumi za uzito wa juu wa wakati huo na akamuuliza kutaka kujua nini huwa kinamtia hamasa zaidi katika kufanya mazoezi kwa bidii.Jibu lake lilikuwa linafurahisha sana pale aliposema-“Kila siku huwa nikitaka kwenda kufanya mazoezi huwa nasikia uchovu na natamani kuendelea kulala,ila huwa najiambia,ni bora niishi kwa sasa kama mtumwa ili nije kuishi kama mfalme hapo baadaye”.Fikra ya namna hii ndio ilimsaidia kufika kule ambako alikuwa anataka kwenda.

Read more

Hatua 3 Za Kukutoa Kwenye Changamoto Unayoipitia Kwa Sasa

Umeshawahi kupitia hali ambayo kila dalili inaonyesha kwamba hautaweza kuinuka tena?Namaanisha mazingira ambayo hata kwa kila anayekuangalia anajua kabisa kuwa hata kama anakutia moyo,hakuna namna unaweza kufanikiwa.Hali hii huwa inaweza kutokea baada ya mtu kuwekeza katika kitu fulani alichokiamini kwa nguvu zote na kisha anakuja kupata hasara ambayo hakuitegemea kabisa,inaweza kutokea pale ambapo mtu uliyempenda sana na kumwamini siku zote anafanya kitu ambacho haukutarajia na kinakuumiza sana moyo,huwa inatokea pale mtu anapopoteza mtu wake wa karibu sana kwa kifo,huwa inatokea pale ambapo unakuwa umefanya kwa bidii kila unachoweza lakini hauoni matokeo,huwa inatokea pale ambapo unaona watu wanaokuzunguka wanafanya kama yaleyale ambayo wewe unayafanya ila hamna matokeo kabisa,huwa inatokea pale ambapo umebakia peke yako na machozi yako hakuna wa kuyafuta,inaweza kutokea pale ambapo umepewa taarifa kuwa ugonjwa wako hauna tiba. Read more