Navigate / search

Mambo 3 Yaliyomsaidia Manny Khoshbin Kutoka Kulala Nje Hadi Kuwa Na Biashara Zake

 

Manny Khoshbin ni mmoja kati ya watu wengi sana ambao wameanzia chini kabisa katika masiha yao na leo wamefika hatua nzuri.Aliingia marekani akiwa na umri wa miaka 14 baada ya kukimbia kutoka katika nchi yake ya Irani ambako kulikuwa na machafuko makubwa sana.

Alipofika marekani alikuwa hawana pesa kabisa na alikuwa hana mahali pa kulala hiyvo iliwalazimu wawe wanalala kwenye gari kabla ya kupata msaada Read more

Adui Wa 7:Kukosa Utayari Wa Kuanza Upya

Adui wa mwisho katika mfululizo huu ambaye amewaangusha watu wengi sana ni ile hali ya kukata tamaa kuanza upya katika maisha yako.Kila mmoja wetu kuna siku na nyakati ambazo anaweza kuzipitia ambazo zinaweza kuonyesha kama vile hakuna tena tumaini la kufanikiwa tena ama kuwa na furaha tena ni kama vile mazingira na hali zote ambazo zinakuzunguka zitaonyesha kuwa hauwezi kuinuka tena,hauwezi kufanikiwa katika ndoot yako,hauwezi kuwa na furaha tena,hauwezi kupiga hatua tena. Read more

Adui Wa 6:Kushindwa Kufanya Mambo Kwa Ubora

 

Kijana mmoja aliyekuwa ni fundi wa nyumba maarufu sana alifanya kazi katika kampuni kwa muda mrefu sana kwa bidii.Baada ya kuona anakaribia kustaafu na hakuna dalili ya yeye kupandishwa cheo wakati wowote,alianza kuwa mzembe wa kazi.Basi zikiwa zimebakia siku chache sana kabla ya muda wake wa kustaafu alipewa kazi nyingine ngumu sana ya kujenga nyumba nzuri ya kisasa.Bosi wake akamwambia kuwa aisimamie na achague anataka kuipendezesha kwa vitu gani,aiwekee swimiing pool bora kabisa na atumie malighafi zozote ambazo anazitaka katika ujenzi.Kwa kuwa alikuwa anajua muda wake wa kustaafu umeshafika na hakuna dalili ya yeye kupanda cheo tena,aliifanya kazi ile kwa uzembe wa hali ya huu sana,alitumia malighafi dhaifu na hakutumia ubunifu katika kuipendezesha. Read more

Adui Wa 5 Kukosa Nidhamu

Watu wengi sana wana vipaji,wana fursa na wana elimu pia lakini kwa sababu ya kukosa nidhamu katika maisha yao wameshidnwa kupiga hatua inavyotakiwa.Nidhamu maana yake ni kufanya kitu ambacho unajua kuwa ni muhimu kwa wakati huo kukifanya aidha unapenda ama la.Nidhamu maana yake hauishi kwa kufanya kinachokupa raha bali unaishi kwa kufanya kilicho muhimu (You don’t live by Convinience but you live by Necessity). Read more

ADUI WA 4: Kukosa Maarifa Yanayotakiwa

Siku zote kiwango cha mafanikio yako kinatokana na kiwango cha maarifa uliyonayo juu ya jambo unalolifanya.Kuwa na malengo na bidii peke yake haitoshi juu ya kile unachofanya,ni lazima ujikite kuwa na maarifa ya kiwango cha juu sana katika kile unachofanya.Itashanagza sana kama wewe unataka kuwa mfanyabishara mkubwa sana lakini kila siku kazi yako ni kusoma magazeti ya udaku tu ama ni kuangalia novie tu.Kama unataka kuwa mfanyabishara mkubwa ni lazima ujikite katika kutafuta elimu na maarifa yahusuyo biashara,tafuta historia za wafanyabiashara waliofanikiwa usome historia zao,ujue vikwazo walivyokutana navyo,ujue mbinu walizotumia kufanikiwa na kukuza makampuni yao. Read more

ADUI WA 3-MAADUI 7 AMBAO LAZIMA UWASHINDE ILI UFANIKIWE

3.Hali ya kukosa mwendelezo katika kufanya mambo(Inconsistency)

Watu wengi mara nyingi sana hufikiri kuwa mafanikio ni matokeo ya kufanya jambo fulani kubwa mara moja na likabadilisha maisha yako.Lakini tafiti zote za mafanikio zimeonyesha kuwa mafanikio mar azote ni matokeo ya mambo madogomadogo ambayo huwa unayafanya kila siku.Kama unataka kubadilisha maisha yako hivyo ni lazima ubadilishe mambo ambayo huwa unayafanya kila siku katika maisha yako. Read more

ADUI WA 2-MAADUI 7 AMBAO LAZIMA UWASHINDE ILI UFANIKIWE

 

Concept of businessman choosing the right door

2.Kushindwa/Kuchelewa kufanya Maamuzi(lack/delay of decision making)

Mark Twain alisema miaka 20 kuanzia leo utajilaumu zaidi kwa mambo ambayo haukuyafanya kuliko yale ambayo uliyafanya (Twenty years from now you will be more disappointed by the things you didn’t do than by the ones you did do).Mara nyingi sana fursa ambazo zinaweza kubadilisha maisha yetu kwa kiwango kikubwa ni zile ambazo zinatuhitaji tufanye maamuzi bila kuchelewa na tuyasimamie maamuzi hayo. Read more

ADUI WA 1-MAADUI 7 AMBAO LAZIMA UWASHINDE ILI UFANIKIWE

MAADUI 7 AMBAO LAZIMA UWASHINDE ILI UFANIKIWE

Moja kati ya misemo Maarufu sana katika bara la Afrika ni ule unaosema,kama hakuna adui aliye ndani yetu basi hakuna adui yeyote wa nje ambaye anaweza kutudhuru kwa namna yoyote ile(If there is no enemy within, the enemy outside can do us no harm).Huu ndio ukweli ambao hauwezi kufichika au kupingwa,kama ukishinda ndani ya moyo wako na kuamini kuwa aweza kufanikiwa basi hakuna kitu/mtu yoyote yule ambaye anaweza kukusababisha usifanikiwe katika maisha yako. Read more

Ufanye Nini Unapokosolewa

Moja ya maneno ambayo siwezi kuyasahau yaliyowahi kusemwa na mwanafalsafa maarufu Aristotle ni pale aliposema-“Kama hautaki kukosolewa,basi amua kutosema chochote,kutofanya chochote na usiwe mtu wa maana,ubaki kuwa wa kawaida”(If you want to avoid criticism,say nothing,do nothing and be nothing).Msemo huu niliufahamu wakati muafaka wa maisha yangu ambapo niliamua kuchukua hatua ambayo watu wengi walikuwa hawaelewi na waliikosoa.

Kitu ambacho nimejifunza kwenye maisha ni kuwa,hakuna namna unaweza kufanya kitu kikubwa ambacho hakijazoeleeka na kila mtu awe upande wako,HAIWEZEKANI.Namna pekee ya kila mtu kukuunga mkono ni pale ambapo utakuwa unafanya kama wao,unasema kama wao na unaishi kama wao.Mara tu utakapoanza kuishi tofauti na wao basi ujiandae kukabiliana na changamoto ya kupingwa.kukosolewa,kusemwa vibaya na hata wakati mwingine kutengwa kabisa. Read more

Sababu Inayokukatisha Tamaa Na Jinsi Ya Kuishinda !!!

Maneno ya Donovan Bailey ni muhimu sana hasa pale aliposema-“Fuata moyo wako unataka nini,jiandae kufanya kazi kwa bidii na kujitoa sana na zaidi ya yote usiruhusu MTU YOYOTE yule akuwekee MIPAKA ya kile ambacho unaweza kukifanya kwenye maisha yako (Follow your passion, be prepared to work hard and sacrifice, and, above all, don’t let anyone limit your dreams).

Siku moja nilipokea simu toka kwa mtu mmoja ambaye kwa hali ya kawaida alikuwa amenizidi kila kitu-Umri,elimu,utajiri na umaarufu.Mtu huyu alinitaka tuonane kwa faragha kwani alikuwa na jambo muhimu sana la kuniambia kwa maelezo ambayo alinipa.Kabla hata sijakutana naye,nilikuwa nina maswali mengi sana kichwani-“Anataka kuniambia nini?” lakini kila nilipojaribu kutafakari sikupata majibu. Read more