Navigate / search

Mbinu Wanayotumia Wanasayansi Wakubwa Kuongeza Uwezo Wao Wa Kufikiri

Kwa mujibu wa mtaalamu wa sayansi ya ubongo,Tony Buzan anasema kuwa kila kmwanadamu ana jumla ya seli bilioni mia moja katika ubongo wake ambazo pia zimeunganishwa na seli zingine elfu ishirini kwa kila mojawapo.Hii maana yake ni kuwa,uwezo wa mtu mmoja kupata mawazo na kuja na mambo ya ubunifu wa aina mbalimbali hayawezi kuzuiwa na kitu chochote kile katika maisha yake.
Inasemwa kuwa kwa mwanadamu wa kawaida huwa anatumia chini ya 2% ya uwezo wake wa ubunifu katika kutatua matatizo yanayomkabili.Kwa mfano mwanasayansi maarufu sana Albert Einstein ambaye alionekana kufanya mambo makubwa sana Read more

Hatua Tatu Ili Uanze Kuishi Ukifanya Kile Unachokipenda

Greer Garson,Mshindi wa wa tuzo ya mwigizaji bora wa kike za mwaka 1943 zinazotolewa na Acdemy award aliwahi kuzungumza kitu muhimu sana kuhusiana na kujenga uwezekano mkubwa wa kuweza kufanikiwa katika maisha yako.Alipoulizwa kuhusuni kitu gani cha kwanza ambacho mtu yoyote anatakiwa kukizingatia anapoanza kuishi ndoto yake alisema:

“Kuanza kufanya kitu kwa sababu unataka pesa ni kosa kubwa katika maisha.Amkua kufanya kitu ambacho unakipenda sana,na kama utakuwa mzuri sana katika kukifanya basi utavutia pesa na utaanza kulipwa”

Nadhani huu ni moja ya ushauri mzuri sana ambao mtu anaweza kuupata kuhusiana na maisha yake.Kuna watu wengi sana katika maisha yao ambao wameshindwa kufika Read more

Jinsi Kanuni Ya Equal Odds Inavyowasaidia Watu Kufanikiwa

Moja ya kanuni muhimu sana katika suala la mafanikio ni kanuni inaitwa “The Rule of equal Odds” ambayo iligunduliwa na mwanasaikolojia maarufu ambaye aliwasoma harvad anayeitwa Keith Simonton.Kanuni hii inasema kuwa chapisho lolote la mwanasayansi ambalo huwa analitoa lina uwezekano wa kufanikiwa sawasawa na chapisho lingine lolote la mwanasayansi mwingine (The average publication of anuy particular scientist does not have any statistically different chance of having more impact than any opther scientist average publication).Kwa maneno mengine hauwezi kujua ni kitu gani ambacho ukikifanya kitakuletea matokeo ambayo unayatarajia. Read more

Jinsi Waliofanikiwa Wanavyotumia Maneno Kutimiza Malengo

Kwenye tamthilia ya “The Brains” inasema kila mwanadamu wa kawaida huwa anajisemea maneno 300 hadi 1000 kwa dakika moja.Haya ni yale maneno ambay huwa anayasema ndani kwa ndani bila nje kusikika.Maneno haya huwa yanaitwa “Self-Talk” yaani kujisemesha wewe mwenyewe.Katika tafiti mbali mbali zimeonyesha kuwa kial self-Talk ambayo unajifanyia huwa ina uwezo wa kukufanya ufanikiwe kama inakuwa
nzuri ama ina uwezo wa kukufanya ufeli kama inakuwa mbaya.Hivi umeshawahi kujikuta unasema maneno ndani kwa ndani na hadi yanakuletea hisia fulani kwenye maisha yako?
Mara nyingi sana watu wamejikuta wakijisemea maneno ambayo yamewafanya Read more

Sababu Kuu 3 Zinazosababisha Watu Kughairisha Mambo

Takribani 80% huwa wanaacha kuendelea na mipango yao waliyojiwekea baada tu ya miezi mitatu ya kwanza mwaka unapoanza.Hii imewafanya watu wengi sana kujikuta wakiwa na hamasa na shauku kubwa mwaka unapoanza na kujikuta shauku yao ikiishia njiani.Unaweza kujikuta kuwa wewe ni mtu ambaye kila mwaka huwa unaanza mwaka kwa kishindo lakini baada ya muda kidogo tu unajikuta umeshakata tamaa na hauendelei tena na kufuatilia utekelezaji wa malengo yako.
Ili usiwe mmoja wa wale ambao kila wakati huwa wanaghairisha mambo na hujikuta wanaanza upya kila wakati ni lazima ujue sababu zinazowafanya watu wengi kuwa na tabia hiyo na wewe ujigundue huwa unaghairisha mambo kwa sababu zipi na ujue namna ya kujitoa kutoka katika tabia hiyo:
Sababu ya kwanza ni kusubiri kuwa na kitu kikubwa ili waanze kufanya kile ambacho wanataka kukifanya.Tatizo kubwa sana ambalo watu wengi sana limewakwamisha ni tabia ya kusubiri kuwa na vingi.SIku zote kumbuka kuwa hauwezi kuwa na vingi kama vile vichache ambavyo unavyo umeshindwa kuvitumia kwa ufanisi.Siku zote kama wewe utakuwa ni mtu wa kudharau kile kidogo ulichonacho basi hautaweza kupata kikubwa unachokitafuta.Kila wakati jiulize-Hivi katika hiki kidogo nilichonacho nitaweza kuanza Read more

Aina 3 Za Marafiki Na Uhusiano Wao Na Mafanikio Yako

Marafiki zako wana nguvu ya kukufanya ufanikiwe ama kukufanya ushindwe kufanikiwa.Kuna watu wengi sana ambao wameshindwa kabisa kufikia katika kilele cha hatima zao kwa sababu tu wameendekeza kuwa na marafiki ambao wamekuwa kikwazo kwa maisha yao.Ila kuna wengine wameshindwa kabisa kufikia kilele cha mafanikio yao kwa kushindwa kutumia vizuri marafiki walionao.Siku zote kumbuka kuwa kila rafiki uliye naye lazima anakuathiri kwa namna fulani-Inawezekana akakuathiri kwa uzuri(Positive) ama akakuathiri kwa ubaya(Negative).Kwa sababu hii,ni lazima kila wakati uwe mtu ambaye unatathmini kuhusu maisha yako na wale wanaokuzunguka na jinsi wanavyochangia kukufanikisha ama kukukwamisha.Katika kitabu changu cha TIMIZA MALENGO YAKO Kwenye mbinu ya 30 nimeeleza mambo 4 ambayo unatakiwa
kuyafanya kuhusiana na kila rafiki uliyenaye ili kuhakikisha kuwa anakuwa msaada badala ya kuwa ni kikwazo kwenye maisha yako,hii inaitwa “Friendship Audit”.

Leo ningependa kuelezea aina za marafiki ambao unawahitaji katika maisha yako kila wakati kama kweli unataka kufanikiwa:
Aina ya kwanza tunawaita marafiki wa kukusukuma katika hatima yako(Destiny Pushers).Hawa ni aina ya marafiki ambao kila wakati watakuja katika maisha yako ili kuhakikisha kuwa hauishii njiani katika kutimiza kile ambacho umekusudia.Destiny Pushers ndio wale ambao mnaweza kupotezana lakini ukiwa katika wakati unataka Read more

Jinsi Ya Kujenga Ujasiri Kwenye Kila Unalofanya

Uwezo wako wa kujiamini na kuwa jasiri kufanya kile ambacho unataka ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa unafanikiwa katika malengo uliyonayo.Kuna watu wengi sana ambao wamepoteza fursa kubwa sana katika maisha kwa sababu walikosa ujasiri,
kuna watu ambao walishindwa kujielezea ili wapate wanachotaka kwa kukosa ujasiri,kuna watu ambao wameshindwa kuanza kufanya kitu wanachokitamani kwa kukosa ujasiri,kuna watu ambao wamefeli usahili wa kazi kwa kukosa ujasiri,kuna watu wameogopa kufanya maamuzi muhimu kwenye maisha yao na matokeo yake wamedumaa mahali pamoja na wanaishi kwa “stress” za hali ya juu kwa sababu ya kukosa ujasiri wa kufanya maamuzi.

Sifa mojawapo ya watu ambao wanafika mbali sana ni wajasiri katika yale ambayo wamekusudia kuyafanya.Huwa wanapoamua kufanya kitu wanachukua hatua bila kuogopa.Kuna watu wengi sana kwa kukosa ujasiri wamejikuta wamekubali kujiingiza
katika “Commitments” ambazo  hawakuwa tayari kuzitekeleza ila kwa sababu ya hofu na uoga wakajiingiza.Kuna watu ambao wamesema ndiyo katika mambo ambayo walikuwa wanatamani kusema hapana na baadaye wakajikuta katika matatizo makubwa sana.Leo nataka ufahamu mambo kadhaa kuhusu hofu katika maisha yako:

Kwanza ni kujua kuwa kila mtu unayemuona ni jasiri katika jambo fulani kwenye maisha yake,kuna siku aliwahi kupata hofu ya jambo hilo.Kila unayemuona leo anasimama mbele za watu na anaongea kwa ujasiri kuna siku alikuwa muoga na alipoitwa mbele za watu pengine alitokwa na jasho jingi kwa uoga.Kila unayemuona huwa akitaka kitu Read more