Navigate / search

Ufanye Nini Unapojikuta Umefanya Kosa Kubwa Maishani

Moja ya tatizo kubwa sana linawalowakabili watu ni hali ya kushindwa kujisamehe baada ya kuwa wamefanya kosa fulani kubwa kwenye maisha yao.Kuna watu ambao wamekosa kujiamini tena katika maisha yao.Kuna watu wanajutia kuwa walichezea fura yao ya kusoma na leo imewasababishia wasiwe watu ambao wana elimu nzuri,kuna watu ambao waliwahi kupendwa sana ila wakapoteza hiyo fursa na leo wameshindwa kuupata ule upendo tena,kuna watu ambao waliwahi kupata pesa nyingi sana na wakazitumia vibaya na leo wako kwenye madeni ama wanaishi maisha magumu n.k
Kwenye maisha angalau kila mtu kuna siku aliwahi kufanya maamuzi fulani ama akachukua hatua fulani ambayo ilimletea majuto ya muda mrefu.Wakati wengine huwa wanaweza kujisamehe na kusonga mbele kuna wengine hali hii huwatesa maisha yao yote na huwasababisha kutokuishi maisha ya furaha na wanakosa hamasa ya Read more

Mambo 3 Ya Kujikumbusha Kila Siku Kama Unataka Kushinda Changamoto

Kila siku unakutana na watu na mazingira ambayo yatakuwa yanatishia sana mafanikio yako aktika kutimiza malengo uliyonayo kwenye maisha.Hii sio wewe tu peke yako,kila mtu ambaye anataka kufanikiwa katika  maisha huwa anakutana sana na hali hii.Kuna changamoto ambazo kila siku zitakuwa kama zinakuambia kuwa hauwezi tena kuendelea mbele hatua moja zaidi.Nimejifunza kuna mambo 3 ya kujikumbusha kila siku kama kweli unataka kubakia kwenye mstari: Read more

Ufanye Nini Kuongeza Kiwango Chako Cha Mafanikio

Christophe Columbus aliwahi kusema “You You can never cross the ocean until you have the courage to lose sight of the shore”(Hauwezi kuvuka bahari kwenda upande wa pili hadi uwe na ujasiri wa kuacha kuangalia ufukwe).Hivi umeshawahi kujiuliza ni kwa nini kuna watu wengi sana ambao wameshindwa kupiga hatua kubwa katika maisha yao na ukiwaangalia wana uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa katika maisha yao?
Hata wewe inawezekana leo uko unafanya kitu ambacho kipo chini kabisa ya uwezo wako lakini umeendelea kufanya tu kwa sababu umehitimisha kuwa hakuna namna Read more

Mbinu Itakayokusaidia Kutatua Kila Changamoto Inayokukabili

Umeshawahi kujiuliza uwezo wa kubuni vitu na kupata suluhisho ya mambo mbalimbali huwa unatoka wapi?Ukweli ni kuwa kila mtu ambaye una muona ana uwezo mkubwa sana katika maisha yake kuna mbinu alitumia ambazo zilimsaidia kuongeza uwezo wake wa ubunifu na uwezo wake wa kutatua matatizo katika maisha,na wewe ukizijua mbinu hizi basi utajijengea uwezo mkubwa sana wa kutatua matatizo katika maisha yako.
Leo nataka nikushirikishe mbinu muhimu ambazo na wewe unaweza kuanza kuzitumia kuongeza uwezo wako wa ubunifu na kupata suluhisho kwenye changamoto zinazokukabili: Read more

Intuition-Mbinu Ya Kukusaidia Kufanya Maamuzi Sahihi Kila Wakati

Umeshawahi kufanya uamuzi fulani katika maisha yako halafu baadaye ukajilaumu sana?Je,katika maamuzi ambayo umeshawahi kujilaumu kuna wakati wowote ambapo ulipata mashaka ya kufanya maamuzi hayo na ukasita ila kwa sababu ya mazingira ya nje ambayo yalioonekana kuwa ni mazuri,ama presha kutoka kwa watu ukaamua kuchukua maamuzi tofauti na moyo wako unavyotaka?
Siku zote kumbuka kuwa wewe kama mwanadamu unapata hisia zaidi ya zile ambazo huwa zinatokana na kusikia,kuona,kuhisi na kunusa.Moyo wako una uwezo wa kupata hisia za mambo tofautitofauti na ni lazima uwe na uwezo wa kuzijua hisia hizo na kuzitafsiri ili ufaidike na kazi ambayo inakufanyia. Read more

Jinsi ya Kujiongezea Thamani Na Kujitofautisha

render of a man with magnifying glass and the text value

Hivi umeshawahi kujiuliza ni jambo gani haswaa unalohitaji kulifanya ili ufanikiwe?Mara nyingi mafanikio yanapotajwa,basi kila mtu huwa anawaza na kufikiria kwa namna tofauti.Ni vyema kujua kuwa ingwa ziko kanuni nyingi za mafanikio ila kuna kitu kimoja ambacho ni lazima uamue mara tu unapoamua kuanza safari ya mafanikio.Kila ambaye unamuona amefanikiwa katika maisha yake kwenye chochote kile ambacho anakifanya sasa,basi ni lazima alizingatia hili tokea mwanzoni sana. Read more

Matokeo Ya Utafiti-Jambo Kubwa Lililowasaidia Watu Wengi Kutimiza Malengo Yao

Kuna watu wengi sana huwa wanadhani kitu ambacho kitawasaidia sana kwenye maisha yao kufanikiwa ni kupewa hamasa kila wakati ili waweze kusonga mbele katika kile kitu ambacho wanakifanya.Hata hivyo kuna siri kubwa sana ambayo kama hautaijua basi kwenye maisha yako yote itakufanya ushindwe kufikia kilele cha mafanikio yako kwa wakati muafaka.Hamasa huwa inakusaidia kuanza jambo ila haina nguvu ya kukufanya uendelee kufanya jambo hilo siku zote,kwa sababu hamasa huwa ina tabia ya kupungua nguvu kadiri muda unavyozidi kwenda. Read more

Hatua 3 Za kubadilisha KIPAJI Chako Kiwe AJIRA Yako

Jim Carrey alianza kuwa na maisha magumu sana tangu akiwa na umri wa miaka 10.Wakati huu maisha yakiwa ni magumu sana aliamua kuanza kufanya kazi ya masaa manane kwa siku kwenye kiwanda fulani ili aweze kupata pesa kidogo za kumsaidia kutimiza mahitaji yake ya kila siku.Alipofika umri wa miaka 14 baba yake ambaye angalau alikuwa ana kipato kidogo ambacho walipokuwa wanachanganya walikuwa wanapata kiasi fulani,alifukuzwa kazi,na hapa maisha yalizidi kuwa magumu sana katika familia. Read more

Njia Rahisi Ya Kujenga Tabia Unayoitaka Kwenye Maisha Yako

Siku moja mwandishi wa kitabu cha namna 100 za kujihamasisha wewe mwenyewe(100 ways to Motivate yourself),steve Chandler alikuwa anafundisha semina kwa wafanyakazi.ILipofika wakati wa mapumziko mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 akamfuata na kuanza kumueleza changamoto zake.

Mzee Yule akamwambia Steve Chandler-“Mimi nina tatizo kubwa sana la kutokumaliza kila ninachoanza katika maisha yangu.Kuna vitu vingi sana nimekuwa navifanya na naishia njiani na siwezi kumaliza.Naomba unisaidie nifanyaje?”.Steve Chandler aliamua kumuuliza anaamini kama yeye ni mtu anayeweza kumaliza mambo akiamua?Mzee Yule alijibu kuwa,haamini kwa sababu hajawahi kumaliza jambo lolote katika maisha yake na hivyo huwa anajiona yeye ni mtu wa kushidnwa kila wakati na hakuna kitu ambacho anaweza kufanya na kumaliza. Read more

Jinsi Ya Kutumia Mbinu ya Commitment Device Ili Kuishinda Tabia Ya Kughairisha Mambo

Moja ya changamoto kubwa sana ambayo lazima uijengee uwezo wa kuishinda katika maisha yako ni tabia ya kughairisha mambo.Tabia hi imewasababisha watu wengi sana washindwe kufikia kiwango kikubwa cha matokeo ya yale wanayofanya kwa sababu kila wakati wamekuwa wanaghairisha mambo muhimu kwenye maisha yao na matokeo yake wanajikuta wanajirundikia mambo mengi sana na huyafanya kwa presha kubwa wakati muda wa mwisho umeshafika(Deadline).

Read more