Navigate / search

Je uko tayari leo kusema “Enough is Enough?”-IMETOSHA.

joel

Siku moja baada ya mtu mmoja kuwa amesoma Makala yangu kwenye gazeti mojawapo ninaloandikia alinipigia simu ili kunieleza jinsi Makala ile ilivyokuwa imemgusa moyo wako.Hata hivyo baada ya kutumia dakika chache kunieleza jinsi ambavyo imemsaidia akaanza kushusha malalamiko jinsi ambavyo yeye amekuwa akifanya kile kitu ambacho nilikiandika kwa muda mrefu sana bila kupata matokeo ya kuridhisha katika maisha yake.Nilipojaribu kumuuliza amekuwa akifanya hivyo kwa muda gani,nilishangaa sana kugundua kuwa alifanya hivyo kwa miezi mitatu tu na tayari ameshaanza kuchoka kwa sababu haoni matokeo. Read more

Vijue Vikwazo Vinavyozuia Kufanikiwa Kwako.

businessmanrollingstone-32avrs4foyzjjhtpg5emtm

Ili uweze kufanikiwa katika malengo yako ni lazima kila wakati utumie muda kujikagua kuona kama kweli uko katika muelekeo wa mafanikio ama kuna mambo ambayo yanakuzuia kuendelea mbele.Ukishayagundua unatakiwa kuyazingatia kwa haraka sana bila kuchelewa.Mambo yanayochelewesha mafanikio yamegawanyika katika makundi makubwa mawili-Moja ni yale ambaye yanatokana na wengine na pili ni yale ambayo yanatokana na wewe mwenyewe. Read more

Je Unaiamini Ndoto Yako Kiasi Gani?

nicks-visiting-his-old-school-in-aus_inside-32ax87mk45ubk8u1iwog7e

Baada ya miaka 50 ya kufanya mafunzo kwa watu elfu ishirini na kufuatilia maendeleo yao katika maisha yao yote,Elmer Letterman alipoulizwa kuhusu kitu kimoja kinachoweza kumfanikisha mtu alisema bila kusita  akasema “intensity of purpose”(Nguvu ya kusudi/Lengo).Hii inamanisha ni uwezo wako wa kuamini kuwa hakuna kitu kinaweza kukuzuia kufikia malengo yako uliyojiwekea,inamaanisha uko tayari kulipa gharama yoyote ilimradi umefanikisha malengo yako.Kuna watu wengi sana ambao nimekutana nao katika maisha yao wana akili,wana fursa,wanafahamiana na watu muhimu,wana elimu n.k lakini kwa sababu tu wamekosa kuwa na malengo thabiti basi wameshindwa kabisa kufikia mafanikio ambayo wengine wanaoonekana kama hawana fursa na uwezo kama wao wamezipata. Read more

Mambo 4 Ya Kufanya Kuhusu Mtandao Wako wa MARAFIKI

Business Communication Duplicate model

Katika mahusiano yako na watu wengine kila wakati utahitajika kufanya tathmini kujua kama uko katika njia sahihi ama la kisha kuchukua hatua stahiki.Kwa ufupi unatakiwa ufanye kitu kinaitwa “Friendship audit” na “Friendship adjustment” yaani ukaguzi wa urafiki ulionao na watu wengine na pia kufanya marekebisho.Hili ni la muhimu kwa kuwa,kila anayeambatana na wewe kwa namna moja ama nyingine anaathiri maisha yako aidha kwa njia nzuri ama mbaya.Hii ndio maana kuna msemo unasema,nionyeshe rafiki zao name nitakuambia wewe ni mtu wa namna gani. Read more