Navigate / search

Hatua 3 Ambazo WAZO Lazima Lipitie Kabla Haujafanikiwa

22

Kuna nyakati katika maisha yetu ambazo huwa tunapitia na ghafla kujikuta imani yetu kubwa tuliyowahi kuwa nayo juu ya mafanikio yetu imekufa.Hivi umeshawahi kuamini katika wazo fulani kwenye maisha yako na mara  baada ya muda fulani unakuta ile nguvu ya kuendelea kuliamini wazo lilelile inazidi kupungua na hatimaye inakufa kabisa?Kuna watu walishawahi kuamini katika wazo fulani la biashara na wakaweka nguvu zao zote katika wazo hilo na wakafanya kila kila kitu ili kufanikiwa walipokuwa wanaanza lakini kwa leo ukikutana nao tena ile hamasa ya kufanya jambo lilelile imeshakufa na wameacha kabisa. Read more

Utafiti wa CHUO Kikuu cha Harvard: Mambo 3 Yanayoleta Mafanikio

Harvard University celebrates Commencement 2014. Spectators watch from the steps of Widener Library. Stephanie Mitchell/Harvard Staff Photographer

Ili kufikia kilele cha ndoto yako na kufanikisha malengo yako yote,ni lazima uwe mtu ambaye kila wakati uko katika hamasa ya kuchukua hatua kuelekea katika lengo kubwa ulilonalo maishani.Kati ya sababu zinazowasababisha watu wengi sana washindwe kufikia malengo yao makubwa ni ile hali ya kuwa leo wako na hamasa kubwa ya kufanya kitu kisha kesho unakuta hamasa imepungua,kesho kutwa wanaanza tena kisha siku inayofuata wamepunguza kasi tena. Read more

Mbinu 2 za Kufanya WATU Wakupe Fursa Zaidi

obama

Wakati Barack Obama ameulizwa kuhusu siri ya mafanikio yake katika eneo la uongozi alijibu “We need to internalize this idea of excellence. Not many folks spend a lot of time trying to be excellent”.Lazima suala la kufanya mambo kwa ubora wa hali ya juu uwe sehemu ya maisha yetu na watu wengi sana huwa hawatumii muda wao mwingi kufanya mambo kwa ubora wa hali ya juu.Watu wengi wameshindwa kufikia hatima za maidha yao kwa sababu ya kushindwa kuwa bora sana kwa kile ambacho wanakifanya. Read more

Ukiwa na TABIA Hii Basi Utaanza kuwa MMOJA wa Watu Waliofanikiwa

nanauka

Gazeti Marufu la Forbes mwaka 2014 lilifanya mahojiano na mabilionea 50 duniani kutoka katika nchi mbalimbali kuhusu bidii yao na masaa ambayo huwa wanayatumia kila siku kufanya kazi.Kati ya kitu kilichoshangaza ni kuwa kati ya hao waliohojiwa asilimia hamsini wanafanya kazi zaidi ya masaa 60 kwa juma(Muda wa kawaida ni masaa 40 kwa juma;yaani maasaa 8 kwa siku tano za juma ukiondoa muda wa saa moja ya mapumziko).Baadhi walionyesha kufanya kazi kwa masaa mengi sana,kama vile mfanyabishara mkubwa sana,Mr.Barron ambaye alisema huwa anafanya kazi takribani kwa masaa 70 hadi 80 kwa wiki. Read more

Njia 3 za Kuishinda Tabia Ya Kughairisha Mambo

88

Zimebaki wiki mbili kabla siku ya mwisho haijafika,hakuna shida bado nina muda wa kutosha sana.Zimebakia siku tatu kabla ya siku ya mwisho,hakuna shida ngoja nimalizie kusoma kitabu cha hadithi na kuangalia filamu inayosisimua mpya iliyotoka hivi karibuni kisha nitamalizia jukumu kabla ya siku ya mwisho haijafika.Imebakia siku moja,kwa kweli muda hautoshi na hivi kwa nini wasisogeze mbele siku ya mwisho.Leo sitaki usumbufu,nitazima simu na nitafanya hii kazi usiku kucha hadi asubuhi niikamilishe.Je,umeshawahi kupitia katika hali kama hii maishani mwako? Read more

Mbinu 3 za Kutumia MUDA wako Ili Kuongeza Kasi ya Mafanikio

time-management

Tangu nianze kufuatilia kuhusiana na sayansi ya mafanikio na historia za watu waliofanikiwa katika maisha yao,hakuna mtu ambaye nimeshawahi kukuta amefanikiwa na asiwe mtu ambaye anajali sana muda.Sifa moja ambayo inawaunganisha watu wote ambao wamefanikiwa katika maisha yao ni uwezo wao wa kuthamini muda na kuamua kuwekeza katika kila dakika waliyonayo.Watu wengi sana wameshindwa kufikia hatima za maisha yao kwa sababu ya kudhindwa kujua namna bora ya kutumia muda wao. Read more

Mbinu 3 za Kupata Maarifa Yatakayofanikisha Malengo Yako

22

Tunaishi katika ulimwengu ambao taarifa mpya zinagunduliwa kila siku.Ukweli ni kwamba kama mtu hatakuwa tayari kujifunza kwa bidii na kila wakati basi atajikuta ameachwa nyuma sana katika eneo lake ambalo ameamua kuwa ndio atatumia muda wake wote katika maisha yake.Siku moja nilikuwa na msikiliza Brian Tracy,mkufunzi maarufu sana wa masuala ya mbinu za mafanikio akasema kuwa kwa ulimwengu wa sasa kila baada ya miaka miwili na nusu maarifa yanapotea na yanakuja mapya kabisa.Hii ikimaanisha kuwa kwa kile uanchokijua leo basi baada ya miaka miwili na nusu kitakuwa hakina manufaa kabisa. Read more

Unasubiri NINI Ili Uanze Kuishi Ndoto Yako?

mENTORSHIP

Mmoja utamkuta anasema bado mambo yangu hayajakaa vizuri nitaanza biashara yangu mwakani,ikifika mwakani anasema tena sasa hivi najipanga nitafanya mwezi wa sita.Mwingine anakuambia nilipanga kufanya kazi miaka 2 tu kisha nijiajiri lakini naona bado ngoja nijipange,matokeo yake amestaafu juzi.Mwingine anasema mimi lengo langu ni kufanya kazi hadi niwe na cheo cha juu kabisa lakini wakati huo nitakuwa namiliki biashara zangu na nitakuwa nafanya kilimo cha kisasa,ni mwaka wa kumi sasa hajaanza kufanya biashara yoyote ile na hata hajanunua bado hata robo heka nje ya mji,anataka kulima kwenye lami? Read more

Hatua 3 za Kufanya Maamuzi Ambayo Yatakuletea MAFANIKIO.

mentorship tz

Mwaka 1973 Profesa Walter Kaufmann wa chuo kikuu cha Princeton aligundua tatizo moja kubwa sana ambalo huwa linachangia watu wengi wasiweze kufanikiwa katika maisha yao.Tatizo hili linaitwa kwa jina la kitaalamu “decidophobia” ikimaanisha hali ya kushindwa/kuwa hofu ya kufanya maamuzi katika maisha.Kwa sababu ya kushindwa kufanya maamuzi watu wengi sana wamejikuta wakiwa katika hali zilezile bila kupiga hatua kwa muda mrefu sana katika maisha yao.Ukweli ni kuwa hali yako uliyonayo leo ni matokeo ya maamuzi ambayo uliyafanya huko nyuma,hivyo kama hautaki kubakia pale ulipo leo ni lazima uamue kufanya aina ya maamuzi ambayo haujawahi kuyafanya kabisa katika maisha yako. Read more