Navigate / search

Jinsi ya Kutumia Wazo Lako La Biashara Kupata Wawekezaji Wakubwa

pixabay-money-2-e1452006248811

Isaac Oboth ni kijana wa miaka 26 ambaye alianza kuishi kama mtoto yatima akiwa na umri mdoog sana.Alipitia katika maisha ya shida na kushindwa kupatiwa mahitaji yake muhimu katika maisha yake hasa yakiwa ni matokeo ya kukosa wazazi na walezi wa karibu.Hata hivyo katika maisha yake yote,Isaac alikataa kabisa kukata tamaa katika maisha yake. Read more

Mbinu 3 Alizozitumia JUSTINA Kujenga Kiwanda Chake Akiwa Bado Ameajiriwa

Justina31

Justina Kavale ni binti wa miaka 33 ambaye akiwa bado ameajiriwa alikuwa na  ndoto ya kuja kujiajiri siku moja katika maisha yake.Wazo lake la kwanza kuhusu biashara alilipata wakati anasoma shahada yake ya uzamili katika utawala wa biashara(Masters in Bussiness Admininstration).Anasema wakati anaendelea kusoma awamu mbalimbali(modules) aligundua kuwa nafasi anayofanyia kazi katika shirika kwa sasa haimruhusu kutumia maarifa yote ambayo anayapata.Hivyo akafikiria kuwa akiwa na kampuni yake mwenyewe basi ataweza kutumia kanuni ambazo amejifunza katika masomo yake. Read more

Jinsi Ya Kutimiza Ndoto Yako Katika Mazingira Magumu

1

Samuel Walton alizaliwa na kukulia katika kipindi kigumu sana cha uchumi nchini marekani(Great Depression),na kwa kuwa familia yake haikuwa ya kitajiri alijikuta anapitia changamoto nyingi sana katika maisha yake ya kila siku.Ili aweze kufanikiwa kuendelea kuishi na kuwasaidia familia yake katika kuongeza kipato alilazimika kufanya kazi za hali ya chini ambazo zinadharauliwa na watu wengi. Read more

Mbinu 3 za Mafanikio Toka Kwa Mwanzilishi wa KFC

kfc

Akiwa na umri wa miaka 5 alifiwa na baba yake na akajikuta alipofikisha miaka 16 basi ameshindwa kabisa kuendelea na shule.Kwa sababu hiyo aliamua kujiingiza katika shughuli mbalimbali za kuajiriwa na ndani ya mwaka mmoja hadi anafikisha miaka 17 alikuwa tayari ameshafukuzwa kwenye kazi nne.Baada ya hapo alijaribu kuomba kujiunga na shule ya sheria lakini alikataliwa na akaamua kuwa wakala wa masuala ya bima na hapo akafeli tena. Read more

Jinsi Unavyoweza Kufanikiwa Ndani ya Muda Mfupi Kama Lufefe

saouth

Leo ukibahatika kufika mitaa ya jiji la Capetown nchini Afrika Kusini na ukaulizia “Mfalme wa Spinachi” basi hakuna shaka utapelekwa moja kwa moja nyumbani kwa Lufefe Nomjana,kijana mwenye umri wa miaka 28 anayemiliki kampuni ya Espinaca Innovations ambayo ni maarufu kwa kutengeneza mikate yenye spinachi na bidhaa zingine zinazotokana na spinachi. Read more

Jinsi Kukosolewa Kunavyoweza Kukusaidia Kufanikiwa Kwa Haraka.

mobbing

Jack Rosenblum aliwahi kusema “If one person tells you you are a horse,he is crazy.If three people tell you,you are a horse there’s a conspiracy afoot. If ten people tell you you’re a horse,it’s time to buy a saddle”(Kama mtu mmoja akikuambia wewe ni farasi atakuwa amechanganyikiwa,watu watatu wakikuambia wewe ni farasi itakuwa ni mbinu wamepanga kukufanyia,ikiwa watu kumi watakuambia wewe ni farasi basi hapo kanunue vile vifaa vinavyotumika kuendeshea farasi kwa sababu utakuwa kweli ni farasi). Read more

JINSI NG’OMBE MMOJA ALIVYOMFANYA VICTORIA AWE MILIONEA

OK Dollars dollar

Victoria kisyombe ana shahada ya kwanza ya mambo ya mifugo na pia shahada ya uzamili katika eneo hilohilo pia aliyoipata chuo kikuu cha Einbur,Uingereza.Maisha yake yalikuwa mazuri hadi pale alipofiwa na mume wake na kubakia majane an watoto watatu wa kuwatunza.Kutokana na mila hakuruhusiwa kurithi kitu chochote ambacho walikuwa nacho wakati mume wake akiwa hai hivyo alinyang’anywa kila kitu.Baada ya hapo Victoria alijikuta amebakiwa na ng’ombe mmoja tu aliyekuwa anaitwa Sero.Akiwa na watoto watatu wa kuwatunza Victoria aliamua kumtumia ng’ombe huyu kuendesha maisha yake na kuwahudumia watoto wake. Read more